kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Binafsi sioni mantiki ya serikali kuhangaika na kupoteza muda na nauli za mabasi kila mwezi wa December ukifika. Huu ni uingiliaji wa kanuni ya biashara inayoitwa "demand and supply in relation to price". LATRA inatia aibu kugeuza kila kitu kuwa siasa na kampeni.
Inajulikana na kufahamika kuwa mabasi yana ratiba zake za kuondoka na kufika ambazo ni fix, ratiba hizi zikikiukwa na wenye magari zinasababisha maredeva na wenye magari kutozwa faini na polisi wa barabarani, mbali na faini za polisi lakini hata wenye mabasi wengine huwa hawaruhusu basi lichelewe kuondoka kwenye muda wake kwasababu ya kugombea abiria ambao ni wachache sana kwenye miezi mingine. Hivyo basi, ratiba za mabasi, faini za traffic, na wamiliki wa mabasi kugombania abiria kituoni inasababisha yafuatayo:
1. Mabasi mengi kuondoka na abiria pungufu (wachache) ambayo ni hasara kwa wenye mabasi.
2. Mabasi kupunguza nauli kama kivutio cha abiria kupanda basi lao, nayo ni hasara
3. Mabasi kufaulisha abiria wao kwenye mabasi mengine na kusitisha safari (hasara) kwa kusosa abiria.
Inapofika December abiria wanakuwa wengi na mabasi machache, na wakati huu bei kubwa ya nauli haisababishi mtu kuacha kusafiri (inelastic) kwakuwa wengi wameshajipanga na kujitayarisha kwa mwaka mzima kuwa desemba lazima aende kwao, no matter how, kiherehere cha LATRA kuzuia bei kupanda na figisu nyingine kwa wenye mabasi ambao sasa wanapata ahueni kwenye biashara yao kinatoka wapi?
Kupanda kwa nauli za mabasi mwezi decemba kuna faida zifuatazo:
1. Wamiliki wa magari wanajaribu kufidia hasara za usafirishaji walizopata wakati wa uhaba wa abiria
2. Kunapunguza ajali za barabarani kwa kuzuia watu wasiokuwa na safari za lazimia kuacha kusafiri wakati huu.
3. Tunatengeneza mabilionea wengi kwenye taifa kwa njia hii
4. Magari mengi yamekopwa, hivyo mikopo kwenye taasisi za fedha inalipwa kipindi hiki.
Binafsi sioni ni kwanini serikali itoe vibari kwa vyombo vya usafiri vingine visivyo na uzoefu wa kusafirisha abiria kwenye njia hizo kusafirisha abiria. Hata TRC haisafirishi abiria miezi mingine kwakuwa hakuna abiria wengi, hivyo wanaogopa kupata hasara na wenyewe. Tuache nguvu za soko ziamue usafiri kwa mwaka mzima, kwani hiyo ndiyo eco-system inavyofanyakazi, survival of the fittest.