LATRA angalieni magari ya Usagara - Mwanza Mjini kwenda Kisesa

LATRA angalieni magari ya Usagara - Mwanza Mjini kwenda Kisesa

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
243
Reaction score
287
Kwa muda sasa imezuka tabia ya baadhi ya madereva wanaoendesha magari yanayofanya ruti ya Usagara kwenda Kisesa, Buswelu, Kisesa, Buzuruga kupitia Mwanza Mjini kupandisha nauli kiholela tofauti na utaratibu unavyoongoza.

Kikawaida nauli ya kutoka Usagara kufika Mwanza Mjini aidha unashukia Stendi ya Posta au Stendi ya Nata nauli unatakiwa ulipe Tsh 600 Mpaka Tsh 700 lakini wanachokifanya dereva na kondakta wake kwa Ruti hizo ni kwamba kuanzia saa moja mpaka saa tatu Asubuhi utaratibu unaotumika wa nauli ni uleule ila ikishafika saa tatu na kuendelea wanasafirisha watu nusu kwa nusu, yaani abiria akipanda gari ya kwenda Mwanza Mjini gari ikifika Buhongwa inakatisha Ruti, kisha wanaanza kupakia abiria upya.

Hivyo, badala ya kusafiri kwa Tsh. 600 kutoka Usagara unajikuta umetumia zaidi ya Tsh. 1000 kwa safari moja, kuna haja Sumatra kuliangalia hili maana maisha ya tulio wengi yako chini na hatuwezi kumudu kutumia Tsh 2000 mpaka Tsh. 3000 kwa usafiri wa kila siku.
 
Back
Top Bottom