Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Siku za hivi karibuni inapofika majira ya Saa Tatu na Usiku niligombana na kondakta wa daladala wakati natoka Kawe kwenda Segerea, alidai nauli ni ni Sjilingi 1,000 badala ya Shilingi 800, akisema kwa sababu ni usiku. Baada ya kuvutana akasusa nauli yangu.
Hii si mara ya kwanza, imekuwa kawaida kulipa Sh 1,000, pia nimeshuhudia abiria wengine wakilalamika tukiwa ndani ya Daladala, kuhusu kupandishiwa nauli kiholela nyakati kama hizo.
Jambo la kushangaza, hakuna tangazo lolote kutoka kwa LATRA linaloruhusu ongezeko la nauli wakati wa usiku. Huu ni uonevu na ni wazi baadhi ya makondakta wanatumia muda wa usiku kuwatoza abiria zaidi bila kufuata taratibu.
Tabia hii siyo tu kwa njia ya Kawe Segerea bali maeneo tofautitofauti ya Dar es Salaam matukio kama hayo ni kawaida, mfano mwingine ni wale wanaopanda Daladala za Mbezi Luis kuelekea Kibaha Mailimoja, nauli ni Sh 700 lakini ikifika kuanzia Saa mbili Usiku nauli inakuwa Sh 1,000.
LATRA mpo? Tunahitaji maelezo na hatua. Usafiri wa umma si biashara ya kubahatisha.