LATRA kupokea maoni ya nauli kuanzia April 8, 2026

LATRA kupokea maoni ya nauli kuanzia April 8, 2026

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) leo itaanza mchakato wa kupokea maoni ya wadau kuhusu uwezekano wa kufanya mapitio ya nauli za usafiri wa umma, baada ya kupanda kwa bei ya mafuta na wadau kulalamika kunachangia kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kwa watoa huduma.

1775547250064.jpeg
Taarifa ya umma iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo jijini Dar es Salaam imesema bei ya mafuta ya petroli na dizeli imeongezeka kwa takribani Sh 950 kwa lita, hali inayotishia kuathiri utoaji wa huduma za usafiri ikiwa haitapatiwa ufumbuzi wa haraka.

Suluo amesema kuwa endapo mwenendo wa kupanda kwa bei ya mafuta utaendelea, ni wazi kuwa gharama za uendeshaji zitaongezeka zaidi na hivyo kuathiri sekta nzima ya usafiri wa umma, jambo linaloweza kusababisha hitaji la kurekebisha nauli ili ziendane na hali halisi ya kiuchumi.

Amefafanua kuwa Latra kwa kuzingatia Kifungu cha 19 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413, ina wajibu wa kufanya mapitio ya tozo mbalimbali za huduma za usafiri, ikiwemo nauli, kwa kuzingatia maslahi ya watumiaji na watoa huduma kwa wakati mmoja.

Kutokana na hali hiyo, mamlaka hiyo imeitisha mkutano wa wadau unaoanza kesho Aprili 8, mwaka huu katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, kuanzia saa 3:30 asubuhi.Suluo amesema lengo ni kukusanya maoni yatakayosaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

​
 
Mbona nauli zishapanda, abood toka dar bukoba ilikuwa 100,000 sasa hivi ni 110,000, kaizerege, katarama zilikuwa 95k, sasa hivi ni 105k..
 
Duh... zile za bungeni kusema kuna vikso vya dharua ili kuangalia wanashushaje mafuta ni mbwembe...Ndo maana yule mbunge alissma bei ya mafuta ni rafiki
 
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) leo itaanza mchakato wa kupokea maoni ya wadau kuhusu uwezekano wa
​
Serikali iweke mafungu kwa ajili ya ruzuku na kuondoa tozo mbali mbali kwenye Lita ya mafuta!
 
LATRA waache haraka kuongeza nauli, vita bado haijaisha.
Na kama lazima kuongeza nauli basi waahidi mafuta yakishuka bei na nauli inapunguzwa
 
Iwe town trip kwa public transport iwe Tshs 7500/-
 
Changamoto Sana hii bei y mafuta ikishuka na nauli zishuke sw. Ila tanganyika kuwa n mtu w zenji kwao nauli ziko pale pale. Uku eti anatukomoa sio kwao Hana cha kupoteza kabisa.
Nimependa tu kua wanachama w fisiem hili ongezeko aliwahusu wao.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom