Congo
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 2,081
- 2,325
Nyie LATRA na TABOA RATIBA zenu za mabasi zinamnufaisha nani. Wananchi hawanufaiki na hawana pa kusemea. TABOA ni chama cha wamiliki wa mabasi sio wasafiri.
Mnaanzisha ratiba za mabasi saa 9 alfajiri. Mnataka wananchi walale MBEZI STENDI. Walale stendi sakafuni kusubiri basi, waende chooni watozwe. Basi lianze usiku, bado lifike linakokwenda usiku. Mmeambiwa wananchi wanataka kuondoka na kufika usiku? Mfano kwa sasa basi kwenda Musoma linaondoka saa 12 asubuhi na kufika Musoma saa 10 alfajiri. Masaa 22.
Likiondoka saa 9 alfajiri litafika saa 7 usiku wa maanani. Anaondoka usiku na kufika usiku.
Kwa nini basi yasiondoke saa 4 asubuhi ili fike saa 2 asubuhi ili wananchi waendelee na safari zao vijijini?
Au ruhusuni mabasi yapange ratiba zao yapendavyo ili mradi yasajili muda wao wa kuondoka. Kuna wananchi wanapenda kuondoka Dar kwenda Mbeya saa 10 jioni baada ya kufanya shughuli zao mchana Dar ili wafike Mbeya asubuhi waendelee na shughuli zao. Hamtaki. Acheni hizo.
Thibitini ajali, mabasi yana vithibiti mwendo, ongeza madereva wawe wawili kwenye mabasi ya safari ndefu.
Acheni hizo.