LATRA na TABOA ratiba zinamnufaisha nani?

LATRA na TABOA ratiba zinamnufaisha nani?

Congo

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2008
Posts
2,081
Reaction score
2,325
Nyie LATRA na TABOA RATIBA zenu za mabasi zinamnufaisha nani. Wananchi hawanufaiki na hawana pa kusemea. TABOA ni chama cha wamiliki wa mabasi sio wasafiri.

Mnaanzisha ratiba za mabasi saa 9 alfajiri. Mnataka wananchi walale MBEZI STENDI. Walale stendi sakafuni kusubiri basi, waende chooni watozwe. Basi lianze usiku, bado lifike linakokwenda usiku. Mmeambiwa wananchi wanataka kuondoka na kufika usiku? Mfano kwa sasa basi kwenda Musoma linaondoka saa 12 asubuhi na kufika Musoma saa 10 alfajiri. Masaa 22.

Likiondoka saa 9 alfajiri litafika saa 7 usiku wa maanani. Anaondoka usiku na kufika usiku.

Kwa nini basi yasiondoke saa 4 asubuhi ili fike saa 2 asubuhi ili wananchi waendelee na safari zao vijijini?

Au ruhusuni mabasi yapange ratiba zao yapendavyo ili mradi yasajili muda wao wa kuondoka. Kuna wananchi wanapenda kuondoka Dar kwenda Mbeya saa 10 jioni baada ya kufanya shughuli zao mchana Dar ili wafike Mbeya asubuhi waendelee na shughuli zao. Hamtaki. Acheni hizo.

Thibitini ajali, mabasi yana vithibiti mwendo, ongeza madereva wawe wawili kwenye mabasi ya safari ndefu.

Acheni hizo.
 
Suala la security njiani ni mihimu pia, usiku uvamizi ni rahisi sanaa
 
Mm nashauri kusiwe na muda wa mabasi kuanza safari, ila 24hrs mabasi yaruhusiwe kuanza safari
 
Suala la security njiani ni mihimu pia, usiku uvamizi ni rahisi sanaa
Nikumbushe basi gani la kwenda bukoba, Musoma, kigoma, ngara, halisafiri usiku kwa sasa? Hiyo kuondoka na kufika si usiku. Unapowaambia basi lianze safari saa 9 si unataka abiria waende stendi usiku? Au huo mchana? Tujadili.
 
Sjui Kwa Njia nyingine lakini root ya dar mbeya huwez kuruhusu basi lisafiri usiku ni hatari sana nyakati za usiku ile njia ina malori mengi Sana na ina ajali nyingi Sana na vulugu za madereva wa basi Kila siku ajali hazitaisha mchana tu mtu kitonga anachoma had malori manne jiulize usiku itakuaje
 
Kama hujui. Kilio kikubwa cha abiria wa Mbeya ni kusafiri usiku. Ila langu la msingi ni kuwa kwa nini mabasi yaanze safari usiku na yamalize safari usiku? Kwa nini abiria wao waishie kwenda na kutoka stendi usiku? Mie nidio hoja yangu kuu.
 
Back
Top Bottom