LATRA, suala la daladala za abiria kubeba mizigo ndiyo utaratibu mpya?

Hebu tupunguzeni chokochoko pasipo na haja ya chokochoko. Sasa mama wa watu ana genge lake Buza, uwezo wake kununua kisanduku kimoja cha nyanya wewe unataka akodishe carry mpaka Buza, ataweza?

Unahisi ule mchicha unaonunua gengeni huko Tabata unafikaje hapo kama sio kupitia daladala hizo hizo?

Sidhani hizo gari zinakosa nafasi za watu kukaa sababu ya hiyo mizigo.

Wacha watu watafute rizki zao kihalali.
 
Hapana boksi la nyanya bei ni 1500 kwa sababu yanakuwa maboksi mengi yanapishushwa vituo mbali mbali.unakuta canter inachukua mizigo ya banana,mombasa ,gongo la mboto mpka chanika huko na kama hivyo mbona mamizigo makubwa yasio ingia kwenye gari kama gunia la vitunguu na kabeji ambayo kimsingi hayana pesa ndiyo wanaleta kwnye magari ya mizigo mkuu usiongee usichokijua kama kitu hujui kaa kimya jifunze.
 
Kwa kirikuu unaeza ambiwa hata 40k, ndio maana konda akikwambia 5000 pamoja na nauli yako inakuwa nafuu kutumia daladala.
Hapana boksi la nyanya bei ni 1500 kwa sababu yanakuwa maboksi mengi yanashushwa vituo mbali mbali.unakuta canter inachukua mizigo ya banana,mombasa ,gongo la mboto mpka chanika huko na kama hivyo mbona mamizigo makubwa yasio ingia kwenye daladala zao kama gunia la vitunguu na kabeji ambayo kimsingi hayana pesa ndiyo wanaleta kwenye magari ya mizigo mkuu usiongee usichokijua kama kitu hujui kaa kimya jifunze.
 
jumatatu asubuhi mkafanye kazi yenu muwanyooshe wale madereva wasiofuata sheria wengine sie wafadhili wetu mia mbili mia tatu wanapata kwa hiyo kazi na wakikosa hizo mia mbili mia tatu na sie huku mtaani twafaa na njaaa.
Mkuu, KEKI ya taifa bado ni kubwa sana. Changamsha Ubongo uache malalamiko.

Hio tabia unaleta inaitwa FITINA, hio ni hatua ya Mwisho binadamu hupitia kabla hajawa MCHAWI kamili.

Kanuni ya Biashara siku zote ni ku-minimize Cost na ku-maximize Profit. Ukiona wanapakia kwenye Daladala ujue Cost iko Low.

Be a Man, Stay Focused.
 
Mtoa mada anatumia mihemko bola kutafakari
 
Mkuu, KEKI ya taifa bado ni kubwa sana. Changamsha Ubongo uache malalamiko.

Hio tabia unaleta inaitwa FITINA, hio ni hatua ya Mwisho binadamu hupitia kabla hajawa MCHAWI kamili.

Be a Man, Stay Focused.
Wabongo sie tuna shida mahali sio bure hasa wewe mtanzania mwenzangu ....hapo uchawi uko wapi kwamba daladala za abiria zibebe mizigo nchi itawalike bila sheria......kuna gari ya tabata ilipakia boksi za nyanya gari ikayumba kidgo abiria akavunjwa mguu na boksi hiyo ni moja ya madhara ya kuweka mizigo na abiria
 
Usafiri wa kuchangia haupo muda wote
 
Wewe ni mchawi. Mizigo ikipakiwa kwenye daladala haifiki? Huo ubongo wako utumie vizuri badala ya kuwaza fitina na kuwaonea wivu watu wa daladala. Hatuwezi kuendelea kwa uwepo wa watu wenye roho mbaya kama wewe.
 
Huyu mtoa mada tayari ni mchawi kamili.
 
Usafiri wa kuchangia haupo muda wote
Haupo muda gani mizigo mingi ya sokoni muda wake wa kutoka inajulikana ni asubui mpka saa 6 muda huo magari yapo mengi tu.......

Wewe nimekwambia kama hujui kitu acha ujuaji kaa kimya jifunze hili swala limekuzidi taarifa nyingi hauna na halijakugusa ndio maana unaropoka ropoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…