Kumekuwa na mkanganyiko wa nauli za daladala zinazotozwa na waedesha/WAMILIKI Daladala mjini Tanga. Kila gari linatoza linavyojifikiria kwa sababu HAKUNA MWONGOZO.
Kagueni magari na hakiki nauli zilizoandikwa ubavuni kama zinafuata viwango vya latra kama zilivyoainishwa katika tangazo la tarehe 17 mwezi Aprili 4 Mwaka 2026.
ONESHENI KWA KILA NJIA:
KILOMITA 10 ZINAISHIA WAPI,
KILOMITA 11-15 ZINAISHIA WAPI , ETC ET ETC
Ni rahisi kudhibiti uholela wa nauli, kinachokosekana na uwajibikaji wa ofisi za LATRA Tanga.
LATRA Dodoma ilioa mwongozo kuhusu nauli za mjini. Mwongozo huo haufuatwi na wamiliki/madereva/makonda wa daladala.
Nauweka Muongozo huo kwa ajili ya rejea.
NAULI ZA MABASI YA MIJINI (DALADALA)
Na Umbali wa Njia Nauli (Tsh.)
1 Usiozidi kilomita 10 …………………………………………………..700
2 Kuanzia kilomita 11 hadi 15………………………………………. 800
3 Kuanzia kilomita 16 hadi 20 ……………………………………….900
4 Kuanzia kilomita 21 hadi 25 ……………………………………..1000
5 Kuanzia kilomita 26 hadi 30 ………………………………………1,200
6 Kuanzia kilomita 31 hadi 35……………………………………… 1,400
7 Kuanzia kilomita 36 hadi 40 ………………………………………1,500
Nauli ya Mwanafunzi
Nauli ya mwanafunzi kwa mabasi ya mijini (daladala) kwa umbali wa njia zote itaendelea kuwa shilingi 200 kwa kila safari.
MAMBO YATAKAYOFUATILIWA NA LATRA
LATRA itafuatilia utekelezaji wa viwango vya nauli vilivyowekwa katika taarifa hii ili kuhakikisha kuwa, mtoa hudumaa.
a) Hatozi nauli inayozidi kiwango kilichowekwa katika taarifa hii;
b) Anatoza nauli kwa kuzingatia umbali, muda au aina ya huduma kama ilivyoainishwa katika taarifa hii;
c) Anaweka wazi viwango vipya vya nauli kwa abiria pale wanapohitaji; na
d) Hamtozi abiria tozo au gharama nyingine yoyote ambayo haijaidhinishwa chini ya taarifa hii.
Imetolewa leo tarehe 17 Mwezi Aprili 4 Mwaka 2026
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI
MAKAO MAKUU - DODOMA