LATRA wamulikeni zaidi Katarama Luxury

LATRA wamulikeni zaidi Katarama Luxury

Yaani wafungie basi kwa sababu USB hazifanyi kazi?

We umetafuta mwenyewe kutukanwa
 
Kwa hiyo ulizungukia siti zote kujaribu kama usb chaja sistimu zinafanya kazi?
 
Wakuu hope mko poa kabisa.

Straight to the topic.

Kama siku kadhaa nyuma LATRA waliwafungia hawa Katarama kutokana na uvunjifu wa taratibu za usafirishaji.

Sasa leo nakuja na malalamiko kuwahusu hawa jamaa kama ifuatavyo.

Mosi siku ya jumatatu nimwsafiri na bus lao (wanaloita vip) kutoka dar kwenda mwanza saa mbili usiku lakini hilo bus halina hadhi ya VIP, usb charging ports bus zima hazifanyi kazi na WAHUDUMU WAKE NI UNPROFESSIONAL kabisa.

Pia, Soma: LATRA yasitisha leseni ya kampuni ya mabasi ya Katarama

Pili leo natoka Mwanza kuja Dar na bus ambalo ilipaswa litoke stand ya NATA saa saba na nusu ila mpaka muda huu saa nane na nusu bus halijafika na maelezo yao bus lipo SCANIA na wameahidi lingefika saa nane kamili.

Sasa hii itapelekea kuanza kukimbia barabarani ili kufidia muda waliopoteza kitu ambacho kinaweza kupelekea ajali zisizo na ulazima

Wito kwenu LATRA, kama hawa watu hawawezi kufuata taratibu ni bora mkawafungia kabisa haina haja ya kua na wasafirishaji wajanja wajanja wasiofuata taratibu.

Nawasilisha.
Luxury huwa hazilalamikiwi, hizo ni bus za kihuni

View: https://web.facebook.com/reel/969701568031552
 
Back
Top Bottom