LATRA yapiga Marufuku Mawakala kukamata au kuwachomolea funguo Bodaboda na Bajaji

LATRA yapiga Marufuku Mawakala kukamata au kuwachomolea funguo Bodaboda na Bajaji

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) imewapiga marufuku mawakala wake kuwakamata madereva wa bajaji na pikipiki, kuwachomolea funguo au kufanya shughuli za utekelezaji wa sheria.

Hatua hiyo inakuja wakati baadhi ya mawakala wakidaiwa kuwavizia madereva katika makutano ya taa za barabarani, kuwachomolea funguo na kuwakamata, hali ambayo wakati mwingine imesababisha ajali kwa madereva na abiria.

Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Dk. Habibu Suluo, amesema hayo leo, Septemba 24, 2026, katika mkutano wa wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Amesema mawakala hao wamepewa jukumu la kutoa huduma za leseni pekee na hawana mamlaka ya kutekeleza sheria dhidi ya madereva.

“Wao ni mawakala wa leseni tu. Utekelezaji wa sheria ni jukumu letu. Wao ni mawakala wa kutoa leseni, si maofisa wa utekelezaji wa sheria,” amesema Dk Suluo.

Amesema Latra itaendelea kutoa mafunzo kwa mawakala wake ili kuwawezesha kuelewa mipaka ya majukumu yao na kuepuka kufanya kazi zilizo nje ya mamlaka waliyopewa.

Soma pia
 
Hao Mawakala wana Taarifa?? mbona pale Gongo la mboto wanaendelea kuchomoa funguo?.
 
Wanachosema na watendaji ni tofauti.. sasa waseme wao latra kwanini wamewapa mawakala wao uwezo wa kujua hii ina latra au haina, na je wakikuta haina latra wafanyaje?
 
Back
Top Bottom