Laughter series: Bibi muone huyu amelala..!

Laughter series: Bibi muone huyu amelala..!

Kwetunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2007
Posts
1,535
Reaction score
412
Siku moja kijana wangu alikuwa mgonjwa, bibi yake akampeleka hospitali moja hapa Dar. Sasa walipokuwa kwenye bench wakisubiri kuhudumiwa, akaja mlemavu mmoja wa macho (kipofu) akakaa karibu yao. Dogo (3.2 yrs old) akaanza kuchezea ile fimbo nyeupe ya yule mlemavu. Bibi yake akawa anamzuia.........ingawaje yule kipofu alikuwa katulia kala pozi.

Sasa dogo akaona mchezo akawa anachukua ile fimbo huku anamwangalia yule mlemavu reaction yake........alipoona kila anachofanya hakuna reaction yeyote......then akamgeukia bibi yake na kumwambia

"BIBI MUONE HUYU AMELALA"
, maskini hakujua kuwa yule jamaa ni kipofu haoni.
 
Back
Top Bottom