Lavalava awekewe mstari wa maelngo wa kuendelea kubaki WCB, Hatuoni maendeleo

Nimeamini masikio yanatofautiana sana ,kiukweli niungane na mtoa mada kuwa sijawahi mwelewa mtu wa kuitwa lava lava hata kwa kujilazimisha imeshindikana ,maajabu sasa kuna huyu wanaemwita mbosso yaan huyu ndo kabisa sijawah penda wimbo wake wowote naona kama anapayuka tu tofaut na alipokuwa yamoto band alikuwa anautendea haki mziki ila saiz hamna kitu sijui kundi lilikuwa linambeba
 
Haka kajamaa vimstari vyake hua vinajirudia sijui kwanini
 
Hupendi miziki ya mahadhi ya pwani
Aina hiyo ya muziki siupendi kwakweli, hakuna wimbo wake nimewahi kuupenda. Yeye, huyo lavalava na kassim mganga.
 
Anaimba kaswida atapata show sana Zanzibar tanga na kilwa
 
Ni bora mara 100 nimsikilize lavalava ila sio Queen darleen
 
Kuna mdau humu jukwaani alishawahi kuandika uzi wenye kichwa cha habari kisemacho; LAVALAVA, BUNDI ALIYETUA WCB.

Nadhani kuna watu watauleta hapa tujikumbushe
 
Kumkodisha harmonize au rayvanny kwa show yaweza kufikia milion 15, Mboso unaweza ikawa milion 7 ila hapa kwa lavalava si ajabu bei za kumkodisha ikawa ni milioni 3
Tatizo lako huna data na unachokiandika
 
Mimi naamini kazi na mchango wa msanii kwenye lebo ni zaidi ya unachokiona kwenye macho. Lava lava ni fundi wa tenzi na uandishi - yawezekana akawa nyuma ya hizo nyimbo nyingi unazozisifia! Kwa mfano Baikoko ni moja kati ya nyimbo alizoandika Lava Lava
 
Nimesikitika sana kuona humuelewi Kassim Mganga, bila shaka wewe ni mpenda singeli (namaanisha miziki ya fujo)
Aina hiyo ya muziki siupendi kwakweli, hakuna wimbo wake nimewahi kuupenda. Yeye, huyo lavalava na kassim mganga.
 
Nimesikitika sana kuona humuelewi Kassim Mganga, bila shaka wewe ni mpenda singeli (namaanisha miziki ya fujo)
Sipendi miziki ya fujo, singeli ndio kabisaaa hata akisikiliza mwingine nakereka.

Sipendi mahadhi ya muziki wanaoimba watu hao.
 
Binafsi napenda muziki wake sana tu, ingawa kuna ukweli kwamba hasongi mbele sijui tatizo ni nini
 
Kuna mdau humu jukwaani alishawahi kuandika uzi wenye kichwa cha habari kisemacho; LAVALAVA, BUNDI ALIYETUA WCB.

Nadhani kuna watu watauleta hapa tujikumbushe
Hahhah hance mtanashati huyo ndo aliandika uzi wa hivyo
 
Mimi nampenda lava lava Ila kuna kitu hakiko right, nadhani mtungaji wa mashairi yake hajampatia bado
 
Kuna k2 hakipo sawa mkuu lava lava naemjua mm anajua sana kuandikaa na kuimba cna shaka na utunz wake n msanii mzuri sema lebo haimtendei haki sio yy haitendei haki lebo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…