chumvichumvi
JF-Expert Member
- May 6, 2010
- 1,207
- 311
Nendeni mkasome taifa bado lina uhitaji wa mawakili.
Mkuu salam, naomba nitofauti nawe kidogo. Japo ni kweli kuwa taifa lina wanasheria wasio kuwa na dhamira safi na maadili ila bado twahitaji wanasheria. Nina sema hivi kwa sababu, mfano kumbuka suala la uvunjwaji wa haki za binadamu nyamuma ni wanasheria(LHRC na wengineo) waliolivalia njuga hadi likafahamika na kuipeleka serikali mahakamani. Pia kuhusu katiba Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS) kwa miaka mingi kimekuwa kikidai mabadiliko ya katiba hii ya sasa. Pia kabla na baada ya muswada wa mabadiliko ya katiba TLS kilitoa waraka kupinga muswada ule 'mbovu', pia walifungua kesi mahakamani kuupinga muswada huofrom my heart bado cjaona umuhimu wa wanasheria nchi hii. Mikataba kibao mibovu inasainiwa na ina vifungu kibao vya kisheria na kila ofisi ina mwanasheria, mswada wa sheria ya katiba umepitishwa kishabiki na mabadiliko mengine ya sheria hufanywa kisiasa na wao wapo. Katiba ya nchi inaendeshwa na mtu anavyotaka mfano suala la uraia wa sioi, uraia wa nchi mbili watu wanao na ni viongozi na katiba haitambui hilo. Watu wanabambikiwa kesi wakiwa mahakamani na wanafungwa. Hayo yote hawayaoni,mpaka sie tuliosoma bachelor of mathematics tupige kelele majukwaani ndo washtuke. Kuna wengine wamesoma na wanategemewa na jamii lakini ukiwasikiliza argument zao kwenye mambo ya kisheria hata mtoto wa first year medicine anamshinda. Wanatetea matumbo yao tu na hawasimamii ukweli mfano werema, tendwa,lubuva, kabudi nk.
vipi kuhus majengo yanayodondoka kama lile la kisutu na chang'ombe house, hii nchi kila kona mbovu. wabunge wenu mnaowapitisha wanafanya mambo kishabiki, hata wanasheria wakiwaambia muswada huo unatatizo wao wapo kishabiki.from my heart bado cjaona umuhimu wa wanasheria nchi hii. Mikataba kibao mibovu inasainiwa na ina vifungu kibao vya kisheria na kila ofisi ina mwanasheria, mswada wa sheria ya katiba umepitishwa kishabiki na mabadiliko mengine ya sheria hufanywa kisiasa na wao wapo. Katiba ya nchi inaendeshwa na mtu anavyotaka mfano suala la uraia wa sioi, uraia wa nchi mbili watu wanao na ni viongozi na katiba haitambui hilo. Watu wanabambikiwa kesi wakiwa mahakamani na wanafungwa. Hayo yote hawayaoni,mpaka sie tuliosoma bachelor of mathematics tupige kelele majukwaani ndo washtuke. Kuna wengine wamesoma na wanategemewa na jamii lakini ukiwasikiliza argument zao kwenye mambo ya kisheria hata mtoto wa first year medicine anamshinda. Wanatetea matumbo yao tu na hawasimamii ukweli mfano werema, tendwa,lubuva, kabudi nk.
Kasahau hata madaktari wanakata kichwa badala ya mguu, na engineers wanabomoa gorofa kwa kuanza chini badala ya juu. Hizo ni challenges ambazo ziko katika kila fani. Lakini huwezi sema yaani huoni kabisa umuhimu wa wanasheria. Uhukumiwe kifo halafu mwanasheria akusemee mahakamani ndio utatambua umuhimu wake.Mkuu salam, naomba nitofauti nawe kidogo. Japo ni kweli kuwa taifa lina wanasheria wasio kuwa na dhamira safi na maadili ila bado twahitaji wanasheria. Nina sema hivi kwa sababu, mfano kumbuka suala la uvunjwaji wa haki za binadamu nyamuma ni wanasheria(LHRC na wengineo) waliolivalia njuga hadi likafahamika na kuipeleka serikali mahakamani. Pia kuhusu katiba Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS) kwa miaka mingi kimekuwa kikidai mabadiliko ya katiba hii ya sasa. Pia kabla na baada ya muswada wa mabadiliko ya katiba TLS kilitoa waraka kupinga muswada ule 'mbovu', pia walifungua kesi mahakamani kuupinga muswada huo
Kuhusu kupitishwa kwa saheria mbovu mkuu waweza laumu wanasheria lakini nadhani watambua kuwa muswada huwa wapitishwa bungeni na kusainiwa na Rais(hiyo mihimili miwili sio wanasheria) ni wanasiasa mara nyingi hawana elimu ya sheria. Umeshajiuliza ni kwanini sheria mbovu zinapitishwa bungeni? Je ni sababu ya wanasheria? Kwangu mimi sababu kubwa ni wananchi, sisi wananchi ndio tunaowachagua viongozi wabovu na walio walarushwa, wao wanatuletea sheria mbovu. Wadhani tukichagua wabunge safi tutapata sheria mbovu? Kumbuka kuwa jamii isiyofikiria vizuri, jamii inayokumbatia viongozi wabovu na kuchagua walarushwa itatoa viongozi wabovu watao tunga sheria mbovu. Kinyume chake kama jamii yetu ikiwa na maadili itachagua viongozi safi watakao tunga sheria nzuri wanasheria watalazimika kutumia sheria nzuri.
Ninakubali kuwa kuna wanasheria wasio na maadili, ila nao ni zao la jamii isiyo na maadili inayowakumbatia. Je hatuna walimu, wahandisi, madaktari n.k wasio na maadili? Kuhusu matumizi ya sheria katika mikataba, japo ni kweli kuwa wanasheria ndio wanaandaa hiyo mikataba, kumbuka kuwa wanaandaa kwa kufuata dondoo za mwajili wao serikali na kuangalia sheria inasemaje, inasikitisha kuona kuwa mikataba mingi 'mibovu' haijavunja sheria za nchi japo kimaadili si mizuri, lakini kisheria, sheria yeyote ni halali mpaka pale itakapofutwa. Mfano Sheria zetu hazisemi mikataba ya biashara kati ya serikali na mwekezaji iingiwaje na hazitoi uwazi katika hilo.
Wanasheria wanahitajika kuwa wengi maana hii itawafanya wasambae sehemu nyingi na huenda ikashusha hata gharama. Ni ukweli usiopingika kuwa wananchi wengi wanaonewa kwa sababu ya kukosa mawakili, umesema kuhusu watu kubambikiwa kesi, kumbuka ukiwa na mwanasheria ni rahisi kushinda kesi uliyobambikiwa kuliko mtu asiye na wakili.
Kiujumla kwangu mimi japo ni kweli wanasheria (baadhi) hawana uzalendo na maadili, nao ni zao la jamii iliyokosa maadili na iliyokosa uzalendo.