Mkuu salam, naomba nitofauti nawe kidogo. Japo ni kweli kuwa taifa lina wanasheria wasio kuwa na dhamira safi na maadili ila bado twahitaji wanasheria. Nina sema hivi kwa sababu, mfano kumbuka suala la uvunjwaji wa haki za binadamu nyamuma ni wanasheria(LHRC na wengineo) waliolivalia njuga hadi likafahamika na kuipeleka serikali mahakamani. Pia kuhusu katiba Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS) kwa miaka mingi kimekuwa kikidai mabadiliko ya katiba hii ya sasa. Pia kabla na baada ya muswada wa mabadiliko ya katiba TLS kilitoa waraka kupinga muswada ule 'mbovu', pia walifungua kesi mahakamani kuupinga muswada huo
Kuhusu kupitishwa kwa saheria mbovu mkuu waweza laumu wanasheria lakini nadhani watambua kuwa muswada huwa wapitishwa bungeni na kusainiwa na Rais(hiyo mihimili miwili sio wanasheria) ni wanasiasa mara nyingi hawana elimu ya sheria. Umeshajiuliza ni kwanini sheria mbovu zinapitishwa bungeni? Je ni sababu ya wanasheria? Kwangu mimi sababu kubwa ni wananchi, sisi wananchi ndio tunaowachagua viongozi wabovu na walio walarushwa, wao wanatuletea sheria mbovu. Wadhani tukichagua wabunge safi tutapata sheria mbovu? Kumbuka kuwa jamii isiyofikiria vizuri, jamii inayokumbatia viongozi wabovu na kuchagua walarushwa itatoa viongozi wabovu watao tunga sheria mbovu. Kinyume chake kama jamii yetu ikiwa na maadili itachagua viongozi safi watakao tunga sheria nzuri wanasheria watalazimika kutumia sheria nzuri.
Ninakubali kuwa kuna wanasheria wasio na maadili, ila nao ni zao la jamii isiyo na maadili inayowakumbatia. Je hatuna walimu, wahandisi, madaktari n.k wasio na maadili? Kuhusu matumizi ya sheria katika mikataba, japo ni kweli kuwa wanasheria ndio wanaandaa hiyo mikataba, kumbuka kuwa wanaandaa kwa kufuata dondoo za mwajili wao serikali na kuangalia sheria inasemaje, inasikitisha kuona kuwa mikataba mingi 'mibovu' haijavunja sheria za nchi japo kimaadili si mizuri, lakini kisheria, sheria yeyote ni halali mpaka pale itakapofutwa. Mfano Sheria zetu hazisemi mikataba ya biashara kati ya serikali na mwekezaji iingiwaje na hazitoi uwazi katika hilo.
Wanasheria wanahitajika kuwa wengi maana hii itawafanya wasambae sehemu nyingi na huenda ikashusha hata gharama. Ni ukweli usiopingika kuwa wananchi wengi wanaonewa kwa sababu ya kukosa mawakili, umesema kuhusu watu kubambikiwa kesi, kumbuka ukiwa na mwanasheria ni rahisi kushinda kesi uliyobambikiwa kuliko mtu asiye na wakili.
Kiujumla kwangu mimi japo ni kweli wanasheria (baadhi) hawana uzalendo na maadili, nao ni zao la jamii iliyokosa maadili na iliyokosa uzalendo.