Lawama na laana ziende Ikulu na sio kwa Rais Samia

Lawama na laana ziende Ikulu na sio kwa Rais Samia

sifi leo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
5,182
Reaction score
8,948
Kauli ya Mkuu wa nchi ya kwamba kazi ya Uraisi ni ngumu inaturudisha enzi za mwendazake maana na yeye alikuwa akitamka mara kwa mara kauli hii.

RAIS Samia ameweka wazi ya kuwa pamoja na ugumu anaokutana nao, yeye kama yeye anashukuru ya kuwa anapata msaada kutoka kwa idara na taasisi mbalimbali zilizomo Ikulu maana zinamsaidia.

Kauli hii ya Rais inaaamanisha kuwa maamuzi mengi mfano kusema kuwa tumpe muda akuze uchumi tutoke tulipo twende pengine ndo aruhusu mjadara wa katiba mpya ni ushauri wa watu wa Ikulu.

Ushauri wa kuvunja Katiba kama walivyokuwa wanafanya yeye na mwendazake wawili tu leo anaufanya yeye na watu wa ikulu mfano kusema mikutano ya siasa isubiri ajenge uchumi,ni mwendelezo wa uvunjaji wa sheria za nchi.

Mifani iko mingi kama uteuzi wa ovyo na mengine sasa lawama na laana ziende Ikulu.
 
Sijakuelewa yaani kiongozi wa eneo asilaumiwe Bali lilaumiwe eneo na wafanyakazi wake?

Unawatenganishaje hawa?
 
Sijakuelewa yaani kiongozi wa eneo asilaumiwe Bali lilaumiwe eneo na wafanyakazi wake??

Unawatenganishaje hawa??
Wapo waliopo ndani ya ikulu wanauzoefu mkubwa kuliko yeye
 
Msurururu wa kuomba teuzi kwa kupitia watu na mafisadi kutaka miradi ndo imeanza kumtia ugumu,kila mtu anataka mwanae/ndugu yake apate teuzi unategemea isiwe ngumu!

Mafisadi nao wanataka favor na shukrani TOKA KWA mama
 
Back
Top Bottom