BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango amesema, Dira ya sasa ilikuwa baada ya mchakato wa miaka mitatu kuanzia mwaka 1997- 99, chini ya uongozi wa Rais Benjamin Mkapa. Na walikuwa wamejiwekea malengo kadhaa. Na tumefanikiwa au hatujafanikiwa?
Mwaka 2000 walisema itakapofika mwaka 2025 maisha ya Watanzania yawe yameboreka Watanzania wawe na maisha bora. Ambayo ilikuwa inapimwa kwa vipimo kadhaa mojawapo ni kipimo cha kipato kwamba ikifika mwaka 2025 kila Mtanzania awe na kipato cha Dola Elfu Tatu kwa wastani kwa mwezi.
Hilo lilikuwa lengo. Nchi ambazo watu wana vipato vya hivyo zinaitwa kipato cha kati (uchumi wa kati)"