LESIRIAMU
JF-Expert Member
- Feb 12, 2008
- 9,006
- 14,536
PDF la Lazaro _ Part 1.
Kwa kuwa Mh Lazaro umerudi CCM, na umerudi kwa kuomba Msamaha, kwa dhati kabisa ukapokelewa pale kwenye mkutano mkuu maalumu wa kumchagua Mwenyekiti wa CCM Taifa, na kwa maelezo yako ni kwamba umeomba radhi kwa uongozi wa CCM na ndo maana umepokelewa. Sawa, naomba hizi tuhuma hapa chini utupatie majibu kwa usawa kabisa, mimi na watanzania wenzangu ambao tungependa kukusikia ukijieleza katika haya mambo yafuatayo.
Tuanzie na haya manne kwanza kwa leo usiku.
1. KUHUSIKA NA UJANGILI
Tarehe 11/4/2012 saa 6 ya usiku gari lillilobeba nyara za serikali lilizuiwa ktk kijiji cha Mwanyonye Singida.
Mtu mmoja ndani ya gari hilo alimtishia kwa bastola afisa mtendaji wa kijiji na badae gari hilo lilivunja kizuizi na kukimbia.
Mkurugenzi mtendaji aliwasiliana TRA na kuambiwa gari hilo no T505 BKM linamilikiwa na mtu aitwaye Lazaro Samwel Nyarandu kwa Tin No. 105-059-701.
Kwa wanaokumbuka kashfa hii iliyosumbua sana na haikuwahi kupatiwa majibu ya haja hasa ikizingatiwa ilimuhusisha waziri Nyalandu kipindi hicho. Hili leo tunaomba ulijibie kwa kuwa uko huru, uko katika chama ambacho unakipenda na kukithamini. Majibu tafadhali.
2. MPANGO WA KUUZA HIFADHI ZA TAIFA
Mpango huu ulitibuliwa na Upinzani na vyombo vya habari. Niseme wazi kipindi hicho nilikuwa nafuatilia mno na kwa ukaribu sana siasa za upinzani kwa maana zilikuwa zina afya kwa jamii maana ziliibua mambo mengi ya msingi tofauti na hizi za Sasa ambazo zinaongozwa na husda, fitna na uongo uongo mwingi.
Nyalandu ulisafiri mpaka South Africa ulikoenda kufanya mazungumzo na kampuni ya African Parks Network (APN). Lengo lilikuwa ni kuikabidhi kampuni hii uendeshaji wa Hifadhi za taifa, Mapori ya akiba na Mapori tengefu.
James Lembeli alikuwa mmoja wa Wakurugenzi wa bodi wa kampuni hiyo APN na huku alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya maliasili na utalii.
Kukiwa na mgongano wa kimaslahi wa wazi na wa kiwango hicho Nyalandu ulishirikiana na Lembeli kuhakikisha kampuni hiyo inapewa hiyo kazi kwa maslahi yenu. Kataa braza, kataa braza.
Nyalandu hukujali hata taarifa za utafiti zilizoonesha namna gani kampuni hiyo imesababisha hasara na uharibifu katika nchi nyingi za Afrika na hivyo kukosa sifa. Mpango huu uliharibiwa na Upinzani ukiongozwa na Chadema na wanahabari hasa Gazeti la Jamhuri. Unabisha? Leo uko katika CCM ambayo Hayati Dr MAGUFULI hayupo, unaweza kutujibu na huwezi kulala nyuma ya NONDO. Tuambie tu braza.
3. TGTS
TGTS ni kampuni ya uwindaji ambayo inamilikiwa na maswahiba wa Nyalandu.
Ukiwa Waziri wa Maliasili ulivunja Sheria kwa maksudi ili kuwapendelea maswahiba wako. Sheria Namba 5 ya wanyamapori ya 2009 inakataza kumilikisha vitalu zaidi ya vitano kwa kampuni moja. Nyalandu uliwapa hawa vitalu 8. Kataa braza, kataa niongeze spana nyingine.
4. LESENI YA RAIS YA UWINDAJI
Hii ni leseni maalum ya uwindaji "Presidential Hunting License". Hutolewa kuwinda bure kwa ajili ya utafiti, shughuli za kiutamaduni, maonyesho, elimu na ikiwa kuna baa la njaa. Mzee ukaamua wewe na aliyekuwa akikutuma utekeleze haya maana hakuwahi kukukemea, maana yake ulikuwa nae kitu kimoja.
Kwanza Nyalandu ulimwondoa ofisini Mkurugenzi wa Wanyamapori Prof. Jaffar Kidegesho na kumteua mwingine, kisha haraka mteule mpya akatia sahihi leseni hiyo na kuruhusu familia moja ya watu 8 ya Marekani ili kuua wanyama 704 wakiwemo tembo 8 kinyume cha sheria na kinyume kabisa na malengo ya leseni ya Rais. Uliitumia leseni ya Rais vibaya. Leseni hii ilitumiwa na familia ya Freidkin ya marekani ambao ni marafiki wa zako hadi sasa.
Na hii ndo ilikuwa gia ya kuwasafirisha wale watoto waliopata ajali kwa kujifanya ni marafiki zako wa chuo fulani huko Marekani, ukatamba sana Mjini, ukasikika sana redioni, ukaonekana mtu nadhifu sana na smart sana, kumbe nyuma ya hiyo safari ya matibabu iligharamiwa na Hayati Dr MAGUFULI ambae leo ndo umesema alilipia gharama hizo zaidi ya 2Bln.
Na familia hii uliyoipa leseni ya Rais kuua wanyama wetu uliongozana nayo Ikulu ikakuombea kwa Hayati Dr MAGUFULI uwe Waziri wa Maliasili, Mzee akasema (NEHI), "HAPANA". Ukakasirika, ukaona utumie loop hole iliyojitokeza baada ya Lissu kupigwa risasi ukakimbia. Maana mzee alikuuliza, hawa wazungu wanakufahamu wewe peke yako tu hapa nchini na hawawafahamu watanzania wengine kwanini? Na kwanini wanahitaji uwe wewe tu ndo washirikiane na Tanzania, ulivyoona hivyo ukaamua kukimbia, haya sasa kwa Sasa hivi ashaondoka, tujibu sisi Watanzania hayo maswali uliyoulizwa na Hayati Dr MAGUFULI.
Spana hizi zitaendelea kesho, PDF sehemu ya 2.
Asante na ninakutakia usiku mwema ukiendelea kujaza hiyo Booklet.
Abdoulquarim Malisa
255[emoji1241]