Lazaro Nyalandu jibu hizi tuhuma

Lazaro Nyalandu alimgaragaza Tundu Lisu kwenye kura za kamati kuu.!

Huyu mzee wa MIGA ,mwanasheria a Acacia anaaminika na nani sasa kama hadi kamati kuu anashindwa kura??

Tundu Lisu ndiyo ajibu tuhuma ,kwa nini alishindwa?
Hiyo mimba usipoitoa itakuua
 
Wewe ni Lazaro Nyalandu?? Haya jibu basi hizo tuhuma acha longo longo.

Chadema kila mara imekuwa ikiwaambia kuwa "ukiona mtu anang'ang'ania gari bovu basi ujue mle kuna mzigo wake"
 
Teh teh politics politics

Ova
 
Hiyo ni moja ya makala. Soma mpaka mwisho, siyo kichwa cha habari tu.

Hata hiyo Title imeandikwa kumgeuka maana yake walikuwa wote. Ukisoma makala utaona alimgeuka kwenye issue moja tu.

Msigwa alikuwa anafanya hadi interviews kumtetea Nyalandu.
Hizo interview zingine hujaziweka humu ili tuzisome wote, ushahidi uliouleta ndio upo tofauti na usemayo.
 
Ila bongo 😂😂 kwahiyo tumeyakumbuka sasa hivi baada ya yeye kurudi CCM ?? KWANINI hatukuhoji akiwa CHADEMA? Au mtu akiwa chadema anakuwa msafi ila akitoka anakuwa mbaya. Kama tuliamua kunyamaza akiwa huku basi kaamua kuondoka tumuache ale maisha 😂. Sema SIASA ZINABOA SANA MUDA MWINGINE
 
Itatuchukua safari ndefu sana kuwa na watu wanaojitambua na upinzani wa dhati.

Kwahiyo huyu homeboy alipokelwa CDM huku wakijua fika haya makandokando yote ila waliamua kumezea tu.

Na hii kumwanika ni kwa vile amerudi CCM?

Mbombo nkafu
 
Sasa kwa maelezo yako nimegundua ndio sababu siku Nyalandu amerudi CCM alikumbatiwa na JK.
 
Kaka uko sawa ,dawa ya jeuri ni kiburi tu,tnasubiria majibu ,asipojibu weka PDF nyingine , mpaka awe mdogo ka pirton
 
Nyimbo haziimbiki upande ule. Nyimbo gani? But to be fair to him, yeye ni mwanasiasa na kama walivyo wanasiasa wote uchwara anatizama kwanza maslahi yake kwanza.

Wanasiasa wengi hawana wanachoamini zaidi ya matumbo yao. Ukiwa na misingi unayosimamia, huwezi kujikuta unahama hama vyama kirahisi namna hiyo.
 
Huyu huenda alikimbilia CHADEMA ili kukwepa mkono wa Magufuli, maana wakati ule Magufuli alikuwa na political capital kubwa nchini,na alikuwa akiwabinya Mafisadi kabla ya yeye naye kugeuka na kuwa mtu wa double standards
Nyalandu akaona akimbilie CHADEMA ili kujipa Kinga ya "Mhanga wa kisiasa" ili akishughulikiwa aonekane kama mtu aliyeonewa!
Lakini TISS wanamjua, Wanajua Ufisadi wake vizuri sana.
 
Sio jukumu la chadema kukamata wahalifu.Hiyo ilitakiwa kua kazi ya vyombo vya dola,kazi ya cdm nikupokea mwanachama awe msafi au mchafu taratibu za chama ziko wazi,hayo mengine viko vyombo vyakushughulikia.Hata hichi kilichowekwa hapa sio andiko la chadema ni jambo la mtu binafsi kwa jinsi alivyoona yeye aweke hayo wazi,sasa wewe kuihusisha chadema inaonnyesha ulivyo kiazi kichwani.
 
sio kazi ya chadema kukamata waharifu!!!!

una matatizo gani wewe??sio jukumu lako kukamata mbakaji,lakini unafahamu unatakiwa kufanya nini??vipi ukimhifadhi nyumbani kwako na ukiwa unajua ni mharifu wa ubakaji???
atakubaka na wewe.
 
sio kazi ya chadema kukamata waharifu!!!!

una matatizo gani wewe??sio jukumu lako kukamata mbakaji,lakini unafahamu unatakiwa kufanya nini??vipi ukimhifadhi nyumbani kwako na ukiwa unajua ni mharifu wa ubakaji???
atakubaka na wewe.
wewe umeshakamata wangapi?.usitake kukigeza chadema chama cha polisi maana hayo mauza uza ya nyalandu yako wazi kila sehemu na yalishasemwa sana.aya sasa karudi ccm ngoja tuone kama mtamkamata.
 
wewe umeshakamata wangapi?.usitake kukigeza chadema chama cha polisi maana hayo mauza uza ya nyalandu yako wazi kila sehemu na yalishasemwa sana.aya sasa karudi ccm ngoja tuone kama mtamkamata.
sijakwambia chadema ni wakamataji,wao ni wakemea uovu.

sasa kama wanataja watu kwa uovu leo,kesho wanamkumbatia kama jamaa yao,chadema ni watu wa namna gani???

achana na ccm hao waliishaamua kukaa mlengo tofauti na nyinyi.
 
Hahahahaha Kataa Blaza, Kataa Blaza, Sasa hapa hujalamba udongo kama yule jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…