Lazaro Nyalandu: Tanzania inahitaji Katiba mpya ili mihimili ya utawala iwe na mipaka iliyo wazi

Lazaro Nyalandu: Tanzania inahitaji Katiba mpya ili mihimili ya utawala iwe na mipaka iliyo wazi

Mudawote: Sasa wewe ndugu utafaidikaje na raslimali za nchi bila miongozo ya katiba? Unafahamu maana ya katiba ya nchi? Hivi mmepeleka wapi akili nyie watu? Wewe unaonaje kama hayo unayofikiri ni mazuri yanayofanywa na mzee wako yakaingizwa na kulindwa na katiba ili hata atakayekuja baadaye ayafuate?
 
Bahati nzuri ni kwamba awamu hii ya Magu inawatafuna wote bila kujali wako upande gani.

Hili ni somo zuri sana kwamba siku nyingine yanapajadiliwa maswala ya kitaifa, vyama vyetu na siasa ziwekwe pembeni.
 
bbc: Kwani kuna ubaya gani kuliona hilo sasa? Ina maana kama hukuona umuhimu wa kumsomesha mtoto wako wa kwanza ukaja kujisahihisha kwa kuelewa umuhimu wa shule kwa mtoto wa pili ni kosa? Binadamu tunaishi kwa kupata maarifa mapya na ufahamu mpya kila kukicha. usishangae ulilolikataa jana leo ukaliunga mkono. Mbona CCM ilikataa mchakato wa katiba mpya mwanzoni lakini baadaya mwenyekiti wa CCM akaunda tume wa katiba chini ya Warioba? Human beings are dynamic not static.
 
Wakati mchakato ulipo pelekwa bungeni huyu mkuu alikuwa Waziri, wakaikoroga wanavyo taka wao. Sasa katiba imembana anataka kutuaminisha kivingine... Hii ni kujifunza kutokana na makosa
Nilishasema huko nyuma hakuna mtu yeyote anayesema mambo ya katiba ni mzalendo hasa akitikea ccm. Huyu Nape Lowasa Sumaye sina hata muda wa kuwasikiliza. Wote ni wanafiki huko nyuma walitetea leo wamebanwa wanajifanya marafiki wa demokrasia. Bashe peke yake ni mzalendo wa kweli hakuna yeyote iwe ukawa. Bashe anamzidi mpaka Lissu na Zitto maana anasema ukweli. Lissu na Zitto wana kachembechembe ka unafiki. Maana huko kwao mmoja akipinga yanayoendelea upinzani wanamwita msaliti sijui demokrasia gani wanaitangaza na kuihubiri.
 
Hakuna anayepinga uwepo wa katiba mpya, ila je vipaumbele vyetu kama taifa kwa sasa ni vipi?? Je ni demokrasia au ni ufaidikaji na rasirimali zetu?

In short katiba mpya kwa sasa siyo agenda ya taifa, maana hata ukiwa na katiba mpya kwa jinsi baadhi ya viongozi wa upinzani (akiwemo na yeye huyu mnafiki nyalandu) uelewa wao wa mambo ni mdogo sana tena sana, na wanaendeshwa na matumbo yao, yaani kama kuna kitu kinashibisha tumbo lake basi atalalia huko huko, ila kama kuna kitu kinasababisha njaa tumbo lake basi atakipinga kweli kweli.

Viongozi wetu wa upinzani hawajitambui kabisa, yaani uelewa wao unaendeshwa na ubinafsi na siyo maslahi mapana ya taifa. Wanataka vile wanavyovitaka wao na siyo inavyovitaka Tanzania, na ndiyo maana kwa kizazi chetu kamwe tusitegemee upinzani kushinda uchaguzi wa rais au kuongoza serikali, maana akili zao zinawaza matumbo na ubinafsi.

Yaani mpaka wachungaji akina Mh. Msigwa hela imewatawala na siyo Tanzania. Wapinzani wetu (including Nyalandu) wapo tayari kushirikiana na mataifa maadui zetu ili kufanikisha ajenda zao. Mungu alisha walaani wapinzani wa Tanzania, na laana hiyo ikae juu yao kwa usaliti na uzandiki. Mungu Mbariki sana tena sana Dkt Magufuli na CCM yetu.
Nimekuunga mkono mpaka ulipoitaja ccm umekoroga. Yanayoendelea kwa magufuli si mambo ya ccm ni Magufuli kama mzalendo huko ccm hakuna anayemuunga mkono ni unafiki tu ndiyo maana unaona wanaungana na wapingaji kutoka upinzani. CCM wanataka hali iendelee kama huko nyuma.
 
Mh. Nyarandu naona ameamua kuja kivingine - Tupo pamoja Kamanda !! Ingawa nina uhakika kabisa kwamba wenzako ndani ya Lumumba hawataki kabisa kusikia hii maneno kwa hoja kwamba "Miluzi mingi.......". Mpaka hapo nafikiri utakuwa umeshajiandaa kisaikologia.
 
Kimachoniuma na kutia hasira, ni kwanini hawayasemi hayo kipindi wakiwa huko, mpaka watibuliwe au kuvurugwa ndio wanapata ufahamu wa jamii inayowazunguka na mahitaji yao.
Kitu kijulikanacho kama UNAFIKI.
 
Wakati mchakato ulipo pelekwa bungeni huyu mkuu alikuwa Waziri, wakaikoroga wanavyo taka wao. Sasa katiba imembana anataka kutuaminisha kivingine... Hii ni kujifunza kutokana na makosa
siku zote mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu,sasa hivi anapiga kelele kwa sababu mkuki umemuingia😀😀😀binadamu bwana.
 
Nimekuunga mkono mpaka ulipoitaja ccm umekoroga. Yanayoendelea kwa magufuli si mambo ya ccm ni Magufuli kama mzalendo huko ccm hakuna anayemuunga mkono ni unafiki tu ndiyo maana unaona wanaungana na wapingaji kutoka upinzani. CCM wanataka hali iendelee kama huko nyuma.
Mkuu nakubaliana na wewe. CCM kuna watu kama Nape, Nyalandu wanataka u-CCM uendelee. Kuna watu kama akina mzee Membe nao pia hawaeleweki. Ila kikubwa nikuambie, wana CCM ni wale wapiga kura wa chini, wananchi wanyonge waliokuwa wanadhulumiwa na wajanja wachache, hao ndiyo CCM tunayoiongelea.
 
Mbunge Nyalandu asema Tz inahitaji katiba mpya ili mihimili iwe na mipaka iliyowazi na kuwepo kwa uangalizi wa Bunge, Mahakama na Serikali.

Huyu jamaa is an agent of the west,sijui Kikwete alifumbwaje macho akamuingiza kwenye serikali yake.To me through his actions he sort of proves to whites that we are indeed a race of low IQ.How for for Gods sake can you be used by the so called investors,but who are actually thugs and looters, collude or conspire against your own people and country.Nyalandu is a traitor like any other,and should be considered as such.
 
Mi nadhani ni kwasababu;

1.Mwenendo wa mkuu haueleweki,wanaogopa atajiongezea mda??!au

2.Kuna watu(wanasiasa wa awamu zilizopita) hawasikiki tena wanataka waibuke upya au,

3.Njaa kali iliyowatawala wanasiasa wanataka posho au

NYIE MNALICHUKULIAJE HILI SUALA??
22687745_898769246955207_7293275651951760761_n.jpg
 
Ni akili tu zimemrudi, na sio Nyalandu peke yake, ni wana CCM wengi, yeye ametangulia tu, wengine watafuata.
 
Back
Top Bottom