PostGE2025 Lazarus Chakwera akutana na tume ya uchunguzi ya matukio ya Oktoba 29,2025

PostGE2025 Lazarus Chakwera akutana na tume ya uchunguzi ya matukio ya Oktoba 29,2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Muwakilishi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola ambaye pia ni Rais mstaafu wa Malawi, Dk Lazarus Chakwera leo Jumamosi, Aprili 11, 2025 , amekutana na kufanya mazungumzo na Tume ya uchunguzi wa Matukio ya vurugu za uchaguzi na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Ujumbe huo wa Jumuiya ya Madola umekutana na Tume hiyo katika ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu, Othuman Chande amesema mazungumzo yao yalijikita zaidi kueleza shughuli za Tume hiyo na Hadidu za rejea za Tume.

Dk Chakwera anaendelea na ziara yake ya kikazi ambayo anataraji kuhitimisha Aprili 16, 2026. Tayari amekutana na kuzungumza na uwakilishi wa vyama Chadema na ACT-Wazalendo.

Pia, amekutana na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu pamoja na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.
 
Yote haya ni matokeo ya Viburi na ulevi wa madaraka wa watu wachache wenye uwezo mdogo wa kupima athari za maamuzi yao.
 
Naona mheshimiwa anaongelea hilo suala kwa ukali, sijui chakwere amemkera😁
 
Back
Top Bottom