Lazima harusi ndo tuishi pamoja?

yetu lini mama?

nukusubiria wewe naona kimya alafu nimesikia yule binti wa jirani tokea uanze kutembea umekaaa ameanza kujipendekeza mwambie nitamtoa jicho asichezeee mali yangu aisee..
 
haina utamu bwana lazima niingie ukumbini bwana
Hayo maisha ya kuiga rafiki ila kama mchumba wako ana pesa hiyo kitu ni lazima ila kama ni za kuhesabika inabidi muende kwa mahesabu kuishi kulingana na kipato chenu mambo ya kukopa kisa harusi hayafai watu wanakopa kukuza mitaji
 
Hayo maisha ya kuiga rafiki ila kama mchumba wako ana pesa hiyo kitu ni lazima ila kama ni za kuhesabika inabidi muende kwa mahesabu kuishi kulingana na kipato chenu mambo ya kukopa kisa harusi hayafai watu wanakopa kukuza mitaji

hapo kwneye kukopa ndio hapana aiseee
 
think +ve.
Hiyo +ve ndo ikoje? uhalisia ni kwamba ndoa siku hizi ni gharama sana wakati pia maisha yako juu mahari unapangiwa mil 2,harusi inagharimu mil 8 na mshahara wako kwa mwezi ni laki 5 how could you afford? kumbuka hiyo inatumika siku moja tu na kuirudisha hiyo pesa mmmh! unafikiri hapo kuna hamasa ya vijana hasa wa kiume kuoa kweli na hapo bado haujakumbana na changamoto za humo kwenye ndoa,watu wataendelea kuzalishana nje ya ndoa tu
 
Nimeulizwa swali hili na mchumba wangu ambae kila kitu tayari ikiwa kupelekana kwa wazazi na mahari tayari. Iii imekaaje jmn!

Nb. Tunabariki tu ndoa kanisani...

Harusi na ndoa ni matukio mawili tofauti yenye maudhui tofauti ingawaje yanafanywa na wahusika wale wale.

Ndoa ni nini?

Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).

Sheria ya Tanzania inafafanua kuwa kuna aina tatu za ndoa zinazokubalika kisheia:
1. Ndoa ya Kidini
2. Ndoa ya Kimila
3. Ndoa ya kiserikali

Harusi ni nini?

Harusi ni sherehe inayoandaliwa na kufanyika ili kuchagiza au kusindikiza tukio la ndoa.

Je kuna ulazima wa harusi?

Hapa inategemea na na utashi wa wahusika, mila, uwezo wa kifedha n.k

Lakini hata kama sherehe za harusi zisipofanyika, ndoa iliyofungwa kwa kufuata misingi ile mitatu pale juu bado itatambulika kisheria.
 
hapo kwneye kukopa ndio hapana aiseee
Heee watu wanakopa mtu unapiga mahesabu unakuta harusi inagharimu mil 7 na kumbuka gharama za harusi ziko juu ya mwanaume na hauwezi kutegemea michango ndo iendeshe harusi yako wewe unaplay pati kubwa kama haujaishia kukopa tu!
 
Konnie mbona kama huyu anaulizia harusi na sio ndoa?

Kumbuka mahari imeshatolewa isipokuwa kuhalalisha mbele ya kadamnasi ndio bado

Hata harusi muhimu, sherehe anasa.
Kama ni wa kanisani wapelekane huko, kama wa msikitini, haya shehe aitwe.
Kama ni wa bomani, mwanasheria achangamshe kalamu fasta, kama ni zile zetu za asili, basi wamtoe kimaso maso akaishi nammewe. Mradi taratibu za kuishi na mumewe bila jicho la hasira la jamii zifuatwe.

Bia na minyama anasa tu, kama zipo haya, kama hazipo sio kisingizio cha kutofunga harusi/ndoa

Kongosho unaniuaaa mie hahhhahha hawa wanaume wetu sijuo mpaka tuwafanyaje maana kwaa akili zao hawawazi kutuoaa, hebu na mie niambie hilo lizombi gani na mie nianze kulala huko ili ndoa itangazwe maana wanaolewaa wengine tu kha!!!hahhhahhhha

Kwa sababu wa kwako sio kichwa ngumu, nakupa huyu, contact person wake ni EMT
 
Last edited by a moderator:
harusi km sherehe au harusi kama process yote inayohusisha mchakato wa kufunga ndoa , then mnamalizia na sherehe ya ndoa???????

ufafanuzi tafadhali...........
 
Mie kanichanganya tu hapo kuwa wanabariki ndoa kanisani!! Sasa dah
 

Loll asijegeuzwa vempire bure nikamkosa wacha nivumilie nikichoka ntasemaa kama dalili hazipo
 
Last edited by a moderator:
Kiruu kiruku mie nalilia uzima cjui kupendwa akinipenda Mungu inatosha na ndoa n lile tedo la papuch na chululu kukorogana na kupakuana mpk mmoja kumzd mwenzie nguvu au cheti ama shela,kwenda mcktn, church nk?
 

Hiyo ya tatu lazima nimtafute
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…