Kipindi cha miaka mitano na ushee, sheria na taratibu nyingi zilivurugwa. Kiufupi heshima juu ya Katiba na Sheria zilipuuzwa na wakati fulani zilitungwa sheria kuhakikisha mafanikio yanapatikana.
Sasa hivi wengi wamezinduka. Wengine waliamua kufungia akili zao makabitini na kutanguliza matumbo yao mbele. Walishiriki katika siasa kandamizi na usigini wa sheria za nchi. Ni kipindi ambacho watumishi wa umma walidhalilishwa kwa kuwekwa ndani na pia maslahi yao yalipuuzwa. Ni kipindi ambacho wafanyabiashara waliogopa kuwa na pesa na bahati mbaya hata wale wakulima wanyonge hawakuwa na sera wezeshi zaidi ya ile ya korosho.
Ili kuanza kuakisi hali halisi ya taratibu na sheria, ni vyema sasa ushirikishwaji wa wafanyabiashara wadogo ufanyike na waanze sasa kuelimishwa taratibu sio kufanya biashara barabarani au mbele ya maduka ya wengine wanaolipa kodi. Miji yote irudi kwenye mpangilio.
Kwa kuwa serikali ilipaza sauti na kuwaita barabarani, sasa ipaze sauti na kuwaita kwenye mijadala na kuwatafutia maeneo ambayo ni salama na endelevu. Hakuna biashara itakayoendelea kwa kuburuza turubai au gunia kupisha gari kisha kurejesha turubai hilo mahali pake. Huu ni mmoja wa uamuzi ambao lazima ufanyike. Haukwepeki.
Ni wakati pia wa kuanza kuweka takwimu zetu kuwa za ukweli. Sekta ya mawasiliano inaonekana kukumbwa na mtikisiko mkubwa sana kutokana na sera zisizo rafiki. Kiashiria hiki na vinginevyo ni kwamba, uchumi huu unapumulia mashine. Si mbaya tukafanya quantitative easing kuongeza mzunguko kwenye pesa na kuangalia vichochezi vya uchumi ambavyo ni rafiki kwa kukuza uchumi.
Tuachane na sera za kujitenga, global isolation. Ukweli hatuna ubavu wa kusimama wenyewe. Tukubali kujifunza na huku tukichukua hatua.