Lazima tuwe na plan ya kupunguza utegemezi wa mafuta

Lazima tuwe na plan ya kupunguza utegemezi wa mafuta

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Nchi zetu hizi za kiafrika ni kama tumelaaniwa, itafika wakati watu wataona aibu kuzaliwa nchi zetu

hazina mipango wala chochote, mipango ni kutazama huduma za jamii basi,

Nikirudi kwenye Hoja, tunahitaji kuwa na mpango wa kuondoka katika utegemezi wa mafuta.

na hapa ni lazima tuweke mkakati katika maeneo yafuatayo
1. Matumizi ya gesi asilia ya kwetu kama mbadala wa mafuta
2. Matumizi ya nishati ya umeme kama mbadala wa mafuta

hapa tunaweza kuwa na mikakati ya mda mfupi na mda mrefu.

vitu kama uagizaji wa magari ili yatumie gesi au ubadilishaji wa yaliyopo ili yatumie gesi sambamba na ujenzi wa vituo vya kujazia gesi ni jambo tunaloweza kufanya ndani ya mda mfupi mpaka kati

matumizi ya vifaa vinavyotumia umeme badala ya mafuta unaweza kuwa mkakati wetu wa mda mrefu
 
Kwa hapa nchini kwetu the best alternative ilikuwa Magari na mitambo mbalimbali kutumia gesi asilia kutoka Mtwara. Lakini kwa jinsi mafuta yaliyowekewa lundo la kodi na serikali (karibia kodi 23 kiasi kwamba jumla ya kodi zote inazidi mpaka bei ya kununua mafuta na kuyasafirisha mpaka bandarini) inaonyesha kwamba ni chanzo kikubwa cha kodi kinachotegemewa na serikali pengine kuliko chochote au labda cha pili baada ya kodi ya kwenye mishahara. Kwa msingi huo sitegemei serikali kwa mfano kuhamasisha matumizi ya gesi asilia kama mbadala wa mafuta. Wewe angalia tuu jinsi usambazaji wa gesi na kuweka mitambo ya LNG ulivyotelekezwa na serikali ya awamu ya tano.
 
Sasa kama tunashindwa kujiondoa katika mafuta hata kutumia gesi yetu basi huo ni umbumbumbu wa viongozi.

kwa mwaka tunatumia more than 4 trilioni kuagiza mafuta

ukiweza kutumia gesi yako maana yake unakuwa na 4 trilioni ya fedha za kigeni ambazo unaweza kuzitumia kufanya mambo mengine ya kimaendeleo.

kama ni kodi si tutazame tuzidistribute vipi kwenye biashara zingine na hata hiyo gesi wekeni kodi hizi huko
 
Back
Top Bottom