Lazio kuzipiku klabu za England kumnasa Samatta?

Lazio kuzipiku klabu za England kumnasa Samatta?

Vhagar

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
20,550
Reaction score
39,949
Lazio kuzipiku klabu za England kumnasa Samatta?



Klabu ya SS Lazio ya nchini Italia imeingia kwenye kipute cha kumnasa mshambuliaji kinara wa klabu ya Genk na timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta.

Samatta amengara sana msimu wa 2018/19 uliokwisha hivi karibuni akiiongoza safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo kuiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi ya Ubelgiji baada ya miaka nane.




Tayari Samatta amekwisha weka wazi kuwa hatarajii kurudi Genk msimu ujao, na ana ndoto za kuhamia katika ligi ya Primia ya England.

Vilabu kadhaa vya England vikiwemo Brighton, Aston Villa, Watford, Leicester na Burnley vimehusishwa na kutaka kumsajili Samatta.

Sasa, klabu hiyo ya Lazio ambao ni miongoni mwa vilabu vikongwe na vyenye mafanikio nchini Italia inaonesha nia ya kutaka kumnyakua mshambuliaji huyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya klabu hiyo iitwayo La Lazio Siamo Noi (Sisi ni Lazio) wanamthaminisha Samatta kuwa na gharama kati ya Euro milioni 10 mpaka 12.

Tovuti hiyo inasema japo Samatta hana mwili mkubwa lakini ana kasi, akili na mzuri kwa mipira ya juu (ya kichwa); "...anaweza kuwa jina (kubwa) la kuliangalia."


Lazio imemaliza katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Serie A katika msimu uliopita na haitashiriki mashindano ya bara Ulaya mwaka uliopita.

Samatta pia anaripotiwa kuzivutia klabu za AS Roma ya Italia na Lyon ya Ufaransa.

Mchezaji huyo na uongozi wake bado wapo kimya juu ya maendeleo ya harakati za usajili.

Hivi Karibuni amesema kuwa atalizungumzia suala la usajili pale muda muafaka utakapofika.




Source bbc swahili
 
Jambo zuri kwake kama kahusishwa na timu kubwa kama lazio.
Nimeona roma na lyon wanamtaka, kama tetesi hizo ni kweli basi asiende uingereza kwa timu km brighton,aston villa sijui nani.. Achague roma ama lyon akikosa huko aende lazio!! Akifeli hapo kwa timu ya uingereza zinazomfukuzia labda Leicester itakuwa move nzuri kwake.
 
Sure mkuu nilipenda kama Everton wangeonyesha nia ingekuwa timu nzuri zaidi.

Ila aende roma. Italy atacheza fresh sana na bila presha kubwa.
Jambo zuri kwake kama kahusishwa na timu kubwa kama lazio.
Nimeona roma na lyon wanamtaka, kama tetesi hizo ni kweli basi asiende uingereza kwa timu km brighton,aston villa sijui nani.. Achague roma ama lyon akikosa huko aende lazio!! Akifeli hapo kwa timu ya uingereza zinazomfukuzia labda Leicester itakuwa move nzuri kwake.
 
Kama alivyofanya wakati ule alipoamua kwenda Genk akitokea Tp Mazembe, hata sasa ni uamuzi wake mwenyewe kuamua wapi pa kwenda. Mimi namtakia mafanikio mema na aendelee kuitangaza nchi yetu kimataifa.
 
bora aende italia ligi haina ushindani sana, pale england kwa Samata ilikuwa ligi ngumu na wangemvunja hata kiuno. SEMA HUKO ITALY RACISM NI ZAIDI YA SPAIN.
 
Natamani aende uingereza kwasababu ndio atatangazwa Sanaa kisha ataweza kuchukuliwa na club kubwa zaidi.

England wana promotions kuliko Italy
 
Back
Top Bottom