the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Jeshi la polisi Mkoani Manyara linawashikilia watumiwa 10 kwa makosa mbalimbali ikiwemo utapeli Kwa kutumia kampuni ya kitapeli ijulikanayo kama Manyara LBL Company Limited inayotoa huduma za kuwekeza na kukopesha fedha kinyume cha sheria na kanuni za Benki Kuu ya Tanzania huku mmoja wa watuhumiwa hao akijihusisha na ulaghai wa kingono na kuwatapeli wanawake kupitia mitandao ya kijamii.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Manyara,SACP Ahmed Makarani amesema katika tukio la ulaghai wa kingono Kijana aliyekamatwa na jeshi hilo ni Victor Onesmo (30) ambapo mtuhumiwa amekuwa akijifanya daktari kisha kuwalaghai wanawake kingono na baadaye kuwaibia simu na vitu vingine.
Source: Clouds Tv
Soma pia :