Le Mutuz case: Ubovu wa Sekta ya Afya Nchini

Ndio lemutuz alikuwa na shida ya moyo ila kuna kuna mambo yalichangia kifo chake.

1: lemutuz anaishi peke yake wenda alipodondoka walinzi walimuona muda umeenda, wenda angekuwa na mke angemkimbiza hata mhimbili na sio mnazi mmoja.
2: ex bf wangu alinifundisha huduma ya kwanza pale mtu anapo dondoka gafla na akasititiza kila mtu anatakiwa kujua hii huduma.
Mtu akidindoka gafla unatakiwa kuweka mikono miwili pale kifuani kwenye moyo na kumshutua kwa nguvu kuamsha mapigo ya moyo. Sasa wale walinzi hata kabla ya kumpekeka hospital ilibidi wajaribu hiyo huduma wenda angezinduka.
Miaka iliyopita nilikuwa natokea mjini nikashuka kituo kimoja nikakuta mmama kadondoka watu wamejaa pale eti wameagiza gari wampeleke hospital.

Moyo ukaniambia sogea pale uone nn kinaendelea nikakuta mmama kalala flat kabisa nikakuta mtu anampepea nikamwambia weka mikono miwili hapo kwenye kifua mpamp kwa nguvu alifanya hilo zoezi kama mara 7 hivi yule mama akatoa sauti mmmmm na kupumua kama mtu aliechoka na akatikisa mguu. Mpaka gari linakuja alikuwa anapumua wakampeleka hospital.

Jamani tunatakiwa kujua hizi huduma za kwanza ndogo ndo ingawa mwisho wa siku Mungu ndio muamuzi.

Lemutuz kuishi peke yake plus stress za mtoto wake kumtukana ndo maana kila siku alikuwa akienda batani may be alikuwa anapunguza stress. Coz angekuwa na mtu wa kumjali alipo kuwa huko batani angeulizwa mbona umechelewa kurudi? Uko wapi? Na alipofika hata angedondoka mkewe ndo angekuwa wa kwanza kujua mme wake hospital ipi inamfaa kutokana na tatizo lake.

Hakuna kitu kibaya kukosa mtu wa karibu wa kukujari.
Apumzike kwa amani maana aliishi maisha ya kusimangwa kisa mtoto wa mchepuko, kila siku yeye ni kuji defend as if alituma maombi azaliwe. Rip lemutuz.
 
Umeongea ukweli.
Pamoja na maisha ya lemutuz kuwa na historia ya sintofahamu lakini hatupaswi kufurahia kifo chake. Aliishi maisha yake japo mengine yaliumiza wengine.

Hapo kituo cha afya kwa mujibu wa wasemaji, palikuwa hamna wahudumu, pengine hata kutokuwa na hiyo mashine wangemkimbiza muhimbili.

Tuseme huyu ni m Tanzania mmoja tu kwa umaarufu wake tumeweza kusikia taarifa zake.

Ni wangapi wanakufa huko mahospitalini kwa kukosa huduma muhimu?

Rest Well .
 
Naunga mkono Hoja, lkn je Le Mutuz alikuwa na mke? Kama alikuwa hana mke namna ya kifo chake kilivyotokea ni sahihi kabsa.
Sidhani km ufahamu wko uko sawasawa kutokuoa na kufa vinahusiana nini! So mtu akiwa kaoa akifa sio sahihi acheni chuki za kijinga
 
Acheni lawama sizizo na msingi

Kwani ni lemutuz pekee yake ndiyo Ana matatizo ya moyo

Kingine lazima muelewe mtu anapokuwa na tatizo lolote mwilini
Inategemea yeye mwenyewe anajisimamia vipi kwenye mambo ya matubabu yake

Je lemutuz alipokuwa na matatizo ya moyo,je alikuwa anahudhuria clinic yake,mambo ya medical checkup
Je alikuwa Ana tumia dawa zake na kufata masharti ya daktari ,kula nk

Hebu nyie patient sehemu za wataalam wa mambo ya cardiologist
Muone jinsi watu wanavyo hudhuria clinic zao

Ova
 
Ana hoja sema kashindwa kuiwasilisha, kea umri wa Lemutuz miaka 62 Jambo la muhimu kwake Ilikuwa ni kukaa karibu na watu na sio lazima awe mke/Mwanamke.
Nafikiri hakutaka kuishi kwenye mila na tamaduni zetu za kuishi kifamilia hata kama si mtoto au mke lakini mara nyingi ndugu wapo wengi wa kuweza kuishi nao, tena kama una uwezo ni raha sana kuchukua ndugu mmoja au wawili wakukulindia boma lako.

Hatari ya kuishi mwenyewe ndio kama hizo ukipata dharura ya shida ya kiafya unaweza kufa huku unajiona maana huna wakukuwahisha hospitali kwenye muda husika. Lakini wanasema kifo hakikosi sababu.
 

Bwana alitoa, bwana ametwaa, watu wa maskini wanakufa kila siku kwa mambi haya, we don't care anymore.
 
Ingawa wanasema alitabiri kifo chake
Lakini maradhi ya moyo huwa wanajua ni kusubiri mda tu
Kweli hakuna atakaeishi milele ila kuna maradhi huwa yanasumbua sana kwa tiba

Hugo Chavez alisema kawekewa sumu na kupata cancer na usa
Alipokuwa anakaribia kufa aliomba ma doctor wafanye juu chini asife wengine wakiwa wabobezi kutoka Cuba
Lakini wapi alikufa tu
Na wa kwetu alikuwa anasema hivi nikifa atakaenirithi ataendeleza?
Unafikiri alikuwa anasema kwa bahati mbaya ?
Alikuwa anajua fika
 

😎😎😎
 
Hospital zetu ni Duni sana.

Nimepita JUZI Muhimbili. Kitengo Cha BOMA na Miuwani.

Jengo limechakaa sanaaaaaaaa.
MIRANGO INAKWANGUA CHINI, NI KELELE MTINDO MMOJA..

VIONGOZI NI WEZI WA KUTUPWA.
YANI NI MAJIZI HASWA.
Boma na miuwani 😆 😆
 
Kiongozi muda wake Boma yee ulikua umefika, tusitafute mchawi nani Mungu angetaka Le mutuz awepo angekuwepo tu, so tumuombee apumzike kwa amani.
Kuwa na mawazo kama haya, yanachangia kwa asilimia kutokuwa na uwajibikaji kwa wattaluma wetu wa afya, na hivyo kusababisha vifo vingi vya wananchi kizembe ambapo vingeweza kuepukwa.
 
Dkt. Magufuli alikuwa mtu wa kufuatilia, vitu kama hivi angeweza kuagiza kila hospital viwepo ila sasa kama kile kifaa cha kupimia tu mambo ya fulani pale ocean road hospital kilichoamriwa kinunuliwe mpaka leo hawajanunua.
Aliviagiza kwenye hospitali ngapi?
 
Haya maneno ya mda kufika ni Africa Tu ..angekuwa Ulaya angekuwa mzima WA fya
Na kwanza huko ulaya na Us, mtu yeyeto akifa tena ghafla kama ndugu yetu Le Mutuz, hata kama ni kapuku, anawekwa kwa muda hospitalini kwa uchunguzi, yaani hii inajulikana sana nchi zote zilizoendelea, ndugu wakienda kumchukua, eti tunataka kuzika leo, wanarudishwa mpaka uchunguzi ujulikane alikufa na matatizo gani na je kulikuwa na jitahada za kumuokoa na pia kama ulikuwepo uwezekano kuweza kuokolewa lakini kuna sehemu uzembe ulifanyika, hapo wahusika lazima, wakajibu kesi kwa Coroner Judge.
Kwa system hii hakuna upuuzi na uzembe sio hapa kwetu watu wnakufa tu, halafu tunamsingizia Mungu kuwa muda wake umefika.
 
Safi sana
Fikiria hata nadhani pale hospitalini hakuna hata aliyejaribu au kuwa na akili ya kufikiria kufanya hivi
Kila mtu muda wake utafika, ni kweli lakini siyo kizembe kama hapa kwetu

Unajua nchi za Ulaya na US, jinsi mfumo unavyofanya kazi, mpaka imefikia, wananchi wanauhuru kuweka kwenye rekodi yake ya afya siku nikipata matatizo yanahitaji kunikoa kwa kutumia hii njia uliofanya inaiitwa CPR(Cardio Pulmonary Resucitation) au kutumia Defibrillator, anaweka saini msinifanyie hivi au msinikoe , niacheni nife. na hospitali inaheshimu huo uamuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…