Le Mutuz: Historia ya kweli juu ya maisha yangu (My American experience)

Le Mutuz: Historia ya kweli juu ya maisha yangu (My American experience)

Kashapata retirement package yake? Kwasababu aliizungumzia Sana kipindi flani humu kuwa ikijakutoka itakuwa kufuru.
 
Kweli Facts ni mwisho wa Polojo. Mwanzoni watu walikuwa wanamkejeli Le mutuz lakini baada ya kuwekwa Facts mezani saa hizi watu wanamtetea na ukitaka kumkejeri utajuta kila mtu yuko upande wake.
Big up Bro.
Mimi binafsi Le mutuz ilikuwa big no-kamwaga facts hapa mpaka nimeomba msamaha-haiwezekani a mere mortal upitie matatizo kama haya na ubaki in one piece
 
Kweli Facts ni mwisho wa Polojo. Mwanzoni watu walikuwa wanamkejeli Le mutuz lakini baada ya kuwekwa Facts mezani saa hizi watu wanamtetea na ukitaka kumkejeri utajuta kila mtu yuko upande wake.
Big up Bro.
Facts za upande mmoja sio fact....
 
Hata aandike kitabu kikubwa kiasi gani haitoshi kuficha maujinga yake anayofanya huyu mzee
 
Ndio ujana ulivyo,full of adventures,ukikuwa ndio unaona mle ulimokosea,lakini wakati mwingine inakuwa too late kurekebisha ulimokosea ila its good kwa ambao ni vijana,maelezo kama haya yanawasaidia kujirekebisha pale ambapo hawaendi sawa,si unajua ujana maji ya moto full of guts,unaona kila kitu unakiweza na utaweza kufanikiwa at your own style...

right on rafiki ,

we all make mistakes in our life, is just some of us they don't want to talk or write about their past
 
Uzuri tumeshakujua wewe ni mmoja wa mashetwani aliokua akipambana nayo Le kokobanga ila umeamua kuja kivingine. Za kuambiwa changanya na za kwako. Pambana na hali yako shetwani wahed!!
Mimi nipambane na Lemutuz ili iwe nini? Le Mutuz hana profile ya kupambana nami
 
Ok hahaha huyu ni my ex mwenyewe saafi saana fanially umekuja hahahaha nilijua huwezi kukosa, ok

1. Kwanza sikuenda kuwaona Pugu, nilienda kuwaona Ukonga/Sitakishari Wewe ukawawahi kua wasinisalimie aliyekuwepo ni dada yako Iku tu, nilikua nimefuatana na Shemeji yako Captain wa Ndege, nilimuambia mapema kilichonileta ni ushahidi tu maana nisingekuja mngenilaumu mpaka kufa kua siwajali watoto. Ndio maana nilikuja na tiketi ya ndege maana nilijua nikiondoka mtakaa kikao cha familia mtanitafuta tukae kikao cha kuhusu watoto. Nilipotoka huko Sitakishari nikapanda ndege Mbeya kwenda kujificha mpaka uondoke, mkaanza kunitafuta na familia yako nikasema nipo Mbeya sirudi Mama yangu anaumwa au umesahau nikamwambia Mama yako mzazi kua sina mpango wa kukaa kikao kujadili watoto wangu, nataka muwaruhusu waje kwangu au bakini nao ila sirudi nilikua nasibiri uondoke kwanza nikarudi na ndege ya usiku baada ya wewe kuondoka na Emirates, hahahahaha

2. Baada ya kuwakataza watoto wasinisalimie wewe ndugu zako mkajipanga getini muone kama nitalia hahahaha nilikua kwenye gari na shemeji yako Captain nilipowaona nikaanza kucheka nakumbuka mlivyopigwa na mshangao kuniona nacheka hahahahaha

3. Siku moja ukawatuma watoto kwa Baba yangu akaniita nikamkatalia nikamuambia watoto wangu siwezi kuwaona kwa kuvizia vizia never, mpaka huyo Mwanamke atakapokubali kua ni wangu au wao wenyewe watakapokua ila kuja kuwaona kwako itakua ni kuwazivizia, SITAKI au umesahau?

4. Mama yangu alipofariki sio wewe uliyewatuma wanitafute hahahaha uliwauliza nilichowajibu au umesahau? wewe chezea wengine sio mimi sina muda wa mchezo na ujinga ujinga,Watoto sio wangu sasa video imekuwataje? hahahaha unayejidhalilisha ni wewe maana unatakiwa kukubali kwamba wewe ni jeuri lakini hapa umekutana na ukuta, halafu nikuulize idea ya kuwabadilisha majina yao uliishia nayo wapi? hahahahahahahahahhaa

5. Imagine kutoka kua mke wangu mpaka kuishia kua mke wa pili na kubadili dini kua musilamu kwa mtoto wa Mchungaji, huoni ni laaana fulani hivi hahahahahhaa nilikuambia Mwanaume kama mimi hand hahahahahhutampata utaishia wanaume second hand huzuni sana hahahahaha

le Mutuz Mobimba

Wanawake wengi ni pasua kichwa.bora ulikimbia mapema mkuu.kama watoto ni wako basi akuletee uishi nao na kuwatunza
 
Mkuu W. J. Malecela nimefurahishwa sana na hii "story" yako, lakini kuna kitu nataka kukushauri hata kama huwa unasema hupendi kushauriwa.

Iko hivi; kwanza achana kabisa na ngono zembe. Kwenye story yako nimeona umegusia mara kadhaa kuwa unamjua sana MUNGU, hivyo kama unalijua NENO la MUNGU kama unavyosema, basi ni lazima ujue kuwa MUNGU, hapendi vitendo vya "uzinzi na uasherati", vitendo ambavyo wewe umekuwa ukivifanya mara kwa mara. Tubu, mwombe MUNGU msamaha, na uanze maisha mapya, na uoe kama ulivyosema kuwa sasa unataka kuoa. Ukioa na kutulia, itakujengea heshima kubwa sana, hasa mbele ya watoto wako.

Pili, watoto wako wameanza kukua sasa, nafikiri mmoja ana miaka 19 kama sijakosea. Kama ni hivyo, huu ni wakati wa wewe kuanza kuwasiliana na watoto wako na kuwa nao karibu hata kama ni kwa njia ya mtandao. Watoto watakuelewa sana kama utaonesha initiative ya kuwa karibu nao kipindi hichi ambacho wanaweza kuchambua wenyewe ipi ni pumba na upi ni mchele. Despite what has happened in the past, but your kids still needs you in one way or another.

Tatu, imefika wakati uachane kabisa na majibizano ya kwenye mitandao na hao unaowaita "mashwetani" wanaotaka kukuangamiza. Ikiwa hutaweza kuacha kujibizana nao, tafadhali sana jaribu kuwa makini sana na vitu unavyo-post hasa picha za "mambebezzz" wako kwani tambua kwamba watoto wako na marafiki zao wanaweza wakawa wanasoma posts zako za mitandaoni, na hiyo itawaadhiri sana watoto wako. Nina uhakika baadhi ya posts ulizoziandika kwenye mitandao zitawaadhiri sana kisaikolijia watoto wako, hasa kama utaendelea kufanya hivyo. Naelewa kwamba "mitandao" ndiyo inakuweka hapa mjini, lakini unaweza kuiendesha kwa akili KUBWA bila kuwaadhiri watoto ambao wanauwezo wa kukufuatilia na kusoma kila kitu.

Nne, usiishie tu kuandika kitabu, ikiwezekana baada ya kutoa kitabu, tafuta mdhamini na utengeneze "movie" itakayohusu historia yako ya kweli ya maisha kuanzia kuwa mtoto wa Waziri Mkuu, kuwa baharia, kwenda New York na kuishi kwa miaka 25 huku ukiwa dereva wa malori, jinsi ulivyokutana na your ex, jinsi mlivyoachana, namna ulivyorudi Bongo na kuanza upya maisha ukiwa na dola 1000 tu, n.k. Naamini hiyo "movie" kama itachezwa vizuri inaweza ikawa ni movie bora kabisa ambayo imewahi kutengenezwa Tanzania kama siyo Africa.

By the way huu ni ushauri tu, na unaweza kuufanyia kazi ama kuupuza. Mimi siku zote huwa napenda sana kuwashauri watu waache maovu, na huwa sijali kama wanasikiliza ama wanadharau. So its up to you to decide bro, but remember this line; "For GOD shall bring every work into judgement, with every secret thing, whether it be good or whether it be evil".
 
Back
Top Bottom