Le Poet Simaro Lutumba astaafu Muziki leo 19.03.2018 akiwa na Miaka 80

Le Poet Simaro Lutumba astaafu Muziki leo 19.03.2018 akiwa na Miaka 80

Masiya,
Kweli weye mtu wa bakulutu,kuya kule fwasi ya FB kwa Baninga ya OK Jazz Friends group
 
Mapumziko mema kwake comrade!!asante sana kwa burudani
 
A-4480277-1469730702-5183.jpeg.jpg

Mwanamziki nguli kutoka nchini Congo DRC mzee Simaro Lutumba maarufu "Masiya" mnamo Jana alitangaza rasmi kustaafu kazi ya mziki alioifanya kwa takribani miaka 60.

Simaro Lutumba alikuwa kiongozi wa band maarufu ya nchini humo iliojulikana kama TP OKK JAZZ ilioanzishwa na marehemu Franco Luambo Makiadi
Simaro Lutumba atakumbukwa kwa utunzi wa nyimbo mbalimbali na mashairi kedekede.

Marehemu Franco kwa kutambua kipaji chake alimteua kuwa Rais wa band hiyo ya OKK JAZZ, Simaro Lutumba mwenye umri wa miaka 80 kwa sasa alifanya tafrija fupi ya kustaafu mziki nyumbani kwake jijini Kinshasa.

Halfa hiyo ilienda sambamba na kukabidhi gitaa lake kwa serikali ikiwa ni ishara ya kustaafu mziki, gitaa hilo lilikabidhiwa kwa mwakilishi wa raisi Joseph Kabila aliemwakilisha katika halfa hiyo.
 
naikubali sana miziki ya zamani
mm n mpenz wa nyimbo za okk jazz
Nina nyimbo 500 ktk sm za okk jazz
simaro lutumba n mtulivu sana hakuwa ana ji exposure KBS nyimbo yake ya Maya naipenda mno
 
Namkubali sana mzee Simaro!haipiti siku 2 sijaisikiliza tungo yake ya Testament ya Bowule, ikiimbwa na Malage de Lugendo.
 
wimbo wake ninaokumbuka sana ni huu


nadhani ndio ulioltea neno PEDESHEE kwenye kiswahili.
 
Back
Top Bottom