Lebanon leo wameamka na majira mawili tofauti ya saa yanayopingana

Lebanon leo wameamka na majira mawili tofauti ya saa yanayopingana

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Wananchi nchini Lebanon wameamka leo wakiwa na majira mawili ya nyakati yanayopingana, huku kukiwa na mzozo kati ya viongozi wa kisiasa na kidini kuhusu ni wakati gani saa zinapaswa kurudishwa ama kusogezwa mbele.

Waziri Mkuu wa Muda Najib Mikati alitangaza kuwa mabadiliko ya yataanza mwishoni mwa mwezi wa Ramadhani mwezi ujao, kuruhusu Waislamu kufungua swaumu ya ya kila siku mapema.

Lakini viongozi wa Kikristo walisema watabadilisha saa kuanzia Jumapili ya mwisho ya mwezi Machi, kama inavyokuwaga katika miaka mingi iliyopita. Shughuli nyingi zimefuata mkondo huo.

Mzozo huo unaonyesha mgawanyiko mkubwa katika nchi hiyo ambapo vikundi vya Wakristo na Waislamu vilianzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe mwishoni mwa miaka ya 1970 na 1980, na ambapo nafasi za kisiasa hugawanya ia miongoni mwa vikundi vya kidini.

Siku ya Alhamisi Bw Mikati, Muislamu wa Kisunni, alitangaza uamuzi wake wa kuchelewesha kuanza kwa uhifadhi wa masaa ya mchana hadi saa sita usiku tarehe 20 Aprili. Hakutoa sababu ya hatua hiyo, lakini wachambuzi wengi wanaiona kama njia ya kuongeza umaarufu wake wakati wa Ramadhani.

Mwezi mtukufu wa Kiislamu ulianza tarehe 22 Machi na kumalizika tarehe 21 Aprili. Ikiwa muda utabaki bila kubadilika, Waislamu wataweza kufuturu saa mapema, saa nyuma, ni kama saa 12 jioni badala ya 1 saa moja ya sasa za za Lebanoni, wakati jua linapozama.

Lakini Kanisa la Christian Maronite nchini Lebanon lenye ushawishi mkubwa lilisema kwamba litapuuza uamuzi huo, na kuuita "wa kushangaza". Mashirika kadhaa makubwa ya Lebanon pia yameamua kupuuza.

Vituo viwili vya habari, LBCI na MTV, vilisogeza saa zao mbele mapema Jumapili. Shirika la ndege la Mashariki ya Kati, ambalo ni shirika la ndege la kitaifa, lenyewe Iilisema saa zake na vifaa vingine vitasalia kufuata majira ya baridi lakini saa zake za safari za ndege zitarekebishwa ili kuepuka kutatiza ratiba za kimataifa.

Kulikuwa na mkanganyiko pia kwa watumiaji wa simu za rununu na vifaa vingine vya kielektroniki ambavyo hubadilika kiotomatiki hadi wakati wa marekebisho ya masaa ya mchana, kwani waendeshaji wengi kuhusu hawakuarifiwa kucheleweshwa kwa wakati.

Chanzo: https://www.bbc.com/swahili/live/65...lS4kc2FFXBRdb-z9Km-M6vP27589t_N-1XNWs7H-TipG4
 
Basi jambo hilo hilo unaweza kukuta damu zinamwagika hapo!
 
Back
Top Bottom