Lebanon sio kigezo cha kufunguliwa kwa mlango wa Hormuz

Lebanon sio kigezo cha kufunguliwa kwa mlango wa Hormuz

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,678
Reaction score
27,653
Lebanon sio kigezo cha kufunguliwa kwa mlango wa Hormuz

Hivyo msidanganywe kwamba Iran imefungua Hormuz sababu ya Lebanon. Hizo ni siasa za kuwatia moyo wasiofikiri ili kuwafanya wasikie nafuu moyoni. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, lazima acheze mchezo ili kupoza harakati.

Aliweka wazi kwenye mitandao ya kijamii leo kuwa uamuzi wa kufungua Hormuz umetokana na sitisho la mapigano kule Lebanon kati ya Israel na Hezbollah.

Viongozi wa Iran wanataka kuonekana kuwa wao ndio "walioishikilia dunia mateka" na wameachia mlango huo kama hisani kwa sababu mshirika wao (Hezbollah) amepata nafuu. Hii inawasaidia kulinda heshima yao (Saving Face) mbele ya wafuasi wao.

Kiini cha mazungumzo ya Israeli na Lebanon

Hoja ya mazungumzo sio baina ya Hezbollah na Israeli bali Lebanon na Israeli. Na Hezbollah imelalamika kutengwa. Na mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya mabalozi wa Israeli na Lebanon yalifanyika jijini Washington, D.C., yakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio mnamo tarehe 14 April.

Shinikizo la Trump na Makubaliano (Aprili 15 - 16, 2026)

Aprili 15: Trump alifanya mfululizo wa simu za shinikizo kwa Rais wa Lebanon, Joseph Aoun, na Waziri Mkuu Netanyahu. Alhamisi, Aprili 16: Trump alitangaza rasmi duniani kote kuwa Israeli na Lebanon zimekubaliana kusitisha vita kwa siku 10 kuanzia saa tano jioni saa za Marekani (EST). Hivyo Iran haikuhusishwa hapo pamoja na Hezbollah mshirika wake. Na moja ya mazungumzo ya Lebanon na Israeli ni kulivunja kundi la Hezbollah. Ndio maana Netanyahu amesema ataendelea kulishambulia kundi hilo. Hivyo mazungumzo haya yapo mkononi mwa Trump, na izingatiwe rais wa Lebanon aliomba sana Marekani iwe mtu kati katika mazungumzo haya na sio Iran ama taifa lolote lile.

Trump: "Kufunguliwa kwa Hormuz Hakuna uhusiano na Lebanon"

Kwa upande wake, Rais Trump amekanusha vikali maelezo hayo ya Araghchi. Trump anadai kuwa Iran imefungua mlango huo kwa sababu ya mzingiro mkali wa kijeshi wa Marekani na hofu ya kupoteza vinu vyao vya nishati. Nukuu ya Trump:

"Dili hili halina uhusiano wowote na Lebanon. Iran imefungua mlango kwa sababu wanajua nini kingetokea wasipofanya hivyo. Tunafanya Lebanon iwe kuu tena, lakini Hormuz imefunguliwa kwa sababu ya 'Transaction' yetu na Iran."

Alisisitiza kuwa Lebanon ipo mkononi mwake," anamaanisha kuwa amefanikiwa kuishinikiza serikali ya Lebanon na jeshi lake (LAF) kuchukua udhibiti zaidi, huku Iran ikishindwa kutoa msaada wa kutosha kwa Hezbollah kutokana na vikwazo na mzingiro wa Hormuz.

Trump anatumia karata ya kiuchumi. Ameahidi mabilioni ya dola kwa ajili ya kuijenga upya Lebanon (Marshall Plan ya Lebanon) kupitia nchi za Kiarabu, lakini kwa sharti moja: Iran itoke nje.

Hoja yake: "Iran haina pesa ya kuwapa ninyi, ina mabomu tu. Mimi nina pesa na amani." Hii inawafanya viongozi wa Lebanon kuanza kumtazama Trump kama mkombozi wa kiuchumi badala ya kufuata maelekezo ya Tehran.

Kama ulivyoona, Waziri Araghchi wa Iran alijaribu kujitapa kuwa wao ndio wamefungua Hormuz kwa ajili ya Lebanon. Trump amepiga chini kauli hiyo kwa kusema kuwa Lebanon imetulia kwa sababu ya mkataba wake wa tarehe 16, na si kwa sababu ya "hisani" ya Iran. Ni vita vya kisaikolojia vya nani ana nguvu zaidi (Who is the Boss?).

Mimi Jeff Massawe

Juzi niliwaambia kwamba kuna mambo yanaendelea kimya kimya lakini kama kawaida yao watu walioungua akili wakabisha na kudai hakuna mazungumzo.

Leo mwelewe kuwa Trump ni mropokaji ndio kama mnavyopenda kusema lakini mtambue ni mropokaji mkweli. Ni nadra sana katika siasa zake anaongea halafu hatendi. Toka ameingia madarakani ameropoka mengi tu na kuyasimamia na yametokea. Juzi usiku alionekana mwenye kujiamini sana na kusema:

"Tuna taarifa, taarifa yenye nguvu sana, kwamba hawatakuwa na silaha za nyuklia kwa zaidi ya miaka 20. Wamekubali karibu kila kitu."

Pia aliongeza kuhusu suala la urani iliyokuwa imefichwa:

"Wamekubali kuturudishia 'vumbi la nyuklia' (nuclear dust) lililozikwa chini ya ardhi kutokana na mashambulizi yetu ya mabomu ya B-2. Iran inataka kufanya dili, na tunashirikiana nao vizuri sana."

Niwakumbushe pia:

Trump mwanzoni alisema ana mawasiliano na mtu wa heshima ndani ya Iran na kupitia yeye kutakuwa na mabadiliko ndani ya Iran. Mossad wakamtaja kuwa ni Mohammed Bagher Qalibaf, spika wa bunge la Iran. Spika alikanusha kweli kweli maana ni aibu. Lakini Trump akazidi kushikilia kuwa mtu huyo wa heshima anatarajia kuongoza mazungumzo. Ajabu dunia ikamwona Galibaf huko Islamabad akinena. Hakika kwenye siasa hakuna ajali. Hivyo tunaweza kuamini sasa maneno ya mwanzo kabisa ya Trump kwamba kuna some regime change ndani ya Iran. Na Vance makamu wa rais wa Marekani naye juzi aliropoka kwamba Galibaf na sio Mojtaba ndio mkuu wa Iran naam anayeiongoza Iran.

Kwahiyo kwa haraka tunaweza kusema Iran haina kifua kikubwa mbele ya Marekani katika mazungumzo haya. Ni jambo la muda tu dunia utapokea habari tofauti za kushangaza.
 
Endelea kupiga kelele hormuz wahuni washaitia tena pini
Yaani huu mwaka mpaka super power wa mchongo atapike nyongo yaani
 
Back
Top Bottom