Ledger Fees Kwenye Mabenki-Makato kwenye Mabenki

Ledger Fees Kwenye Mabenki-Makato kwenye Mabenki

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,973
Reaction score
6,750
Habari za wakati huu;
Ni matumiani yangu kwamba mnaendelea salama na shughuli za ujenzi wa Taifa letu;

Ni muda mrefu sana sijaweka andiko hapa jukwaani hivyo basi leo nimeona nichokoze mjadala kidogo kuhusu haya makato ambayo yanaitwa ledger Fees ambayo hutozwa na Mabenki mbalimbali yakiwa na wastani wa kati ya Shilingi 1000 kwa mwezi had shilingi 60,000 kwa mwezi kwa kutegemea aina ya akaunti na aina ya Benki.

Kwa Tanzania Benki pekee ambayo naifahamu ambayo haina haya makato ya kila mwezi ni Benki ya Equity.Kama kuna Benki nyingine tunaweza ambiana hapa ili tufahamu zaidi.

Lengo la mjadala huu ni kufahamu;

1. Je Makato hayo yanaathiri kwa kiasi gani Ufikiaji wa Huduma za kibenki kwa jamii kwa ujumla?
Kwa mtazamo wangu naona makato haya yanaathiri sana watu kutumia Mabenki.Ndio maana watu wengi wanona bora zaidi kuweka Pesa zao kwenye Mitandao ya SIMU ambapo angalau ukiondoa zile ada za utoaji Pesa basa Pesa yako inaendelea kubaki kama ulivyoiweka.


2. Je wewe kama mfanyabiashara huwa unazingatia makato ya benki unapotaka kufungua akaunti katika benki fulani?

Kwangu mm ni swala la muhimu sana,Ninapoenda Benki huwa nauliza gharama za uendeshaji wa kaunti kuanzia makato na gharama nyingine.Nikiona zipo huwa nafikiria mara mabili iwapo ni lazima niwe na akaunti benki hiyo

Je ni mambo gani ambayo huwa unazingatia unapotaka kufungua akaunti ya benki kwa matumizi binafsi au matumizi ya kibiashara.

Binafsi huwa nazingatia Gharama za kuendesha akaunti husika,Upatikanaji wa huduma mfano matawi na alternative Banking Channels,Gharama za Mikopo na Huduma nyingine za Kifedha.

Kimsingi unapotaka kufungua akaunti benki lazima ujiulize maswali mengi kwa kutegemea aina ya biashara na aina ya wateja wako ambao watakulipa na wale uatakaowalipa.

Karibu tujadili kwa taratibu na kujifunza kwa pamoja
 
Back
Top Bottom