Wo shi niubi
JF-Expert Member
- Aug 14, 2015
- 1,353
- 1,784
Sijakulia wakati wa mwinyi wala Nyerere lakini historia ndo inatuongoza na kutupatia mwanga kwa vijana wengi ambao hatukuwa wakati ule, kulingana na maoni ya watu wengi, mwinyi alikuja kuifungua Tanzania ni vyema sana, lakini huwezi kufungua nchi kwa kuruhusu tu kuingiza kila kitu nchini maana yake kwanza utaua hata kidogo kilichopo, pili utaua thamani ya pesa yako nchini, tatu utajenga taifa tegemezi, yaani watu wataka mkao wa kusubiri/au kuletewa, Nne utaondoa uzalendo ya bidhaa za ndani dhidi ya bizaa za kigeni, madahara yake ni kuwa na Taifa linalowaza sana msaada hata kwa kitu kidogo hapo ni ndoto kuendelea na mataifa makubwa yakiona hivyo hufurahi sana.
Kuna tofauti kubwa sana ya economic reform ya watu wa china na mzee mwinyi, china ilifanana sana kisera na Tanzania, lakini wao walivyofanya reform ilikuwa tofauti kabisa na ya mzee mwinyi, wao waifanya reform ya Kilimo na viwanda + kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi, hivyo wakaanza kutenga maeneo kwa ajiri ya wawekezaji kutoka nje, wakaja kujenga viwanda, wakati huo huo serikali ya china ilijikita zaidi kugawa maeneo kwa wananchi wao ili waweze kulima kilimo cha kisasa, ndo kile kipindi watu wote waliomaliza vyuo kwa course za kilimo walikuwa wanapelekwa vijijini kusimamia kilimo na wakipata mali ghafi zinakwenda moja kwa moja viwandani, hivyo viwanda vikasimama vya wazawa , pia viwanda vikasimama vya wageni waliotoka , wao wakaanza kuuza bidhaa kwa raia wao pia nje ya nchi.
Kuna kitu kimoja pia tunatakiwa tuelewe, toka Enzi za Mao china imekuwa na viwanda, 80% ya viwada vilikuwa vinamilikiwa na serikali ya china kama ilivyokuwa kuwa Tanzania na ufanisi wake ulikuwa sio mdogo, baada ya 1978 walipojifungua hawakuviacha au kuviua viwanda vyao bali walivibinafsisha tu ili kuongeza uzalishaji, serikali ikawa inakusanya mapato, hakuruhusu vitu kuingia nchi kwao kiholela.
Kingine, serikali ilianza kukopa kutoka Bank ya dunia kwa ajiri ya kujenga miundo mbinu ya kisasa kuconnect the whole country na wakasimamia kwa makini, watu wakaanza kufanya biashara nchini bila vikwazo then wakafunguka hadi nje ya nchi. Maendeleo ya china kwa style ile iliwachukua ndani ya miaka 14 tu kila kitu kilikuwa kimeeleweka.
Swali je kufunguka kwa mzee mwinyi ilikuwa ni same same kama watu wa china? Jibu ni NO, je mwinyi alijenga kiwanda au alianzisha mchakato wowote wa kuondoa umasikini kama watu wa china walivyofanya, jibu ni NO, Je kuna barabara zilizojengwa kuunganisha nchi ya Tanzania jibu ni NO,inawezekana kabisa hata sarafu ya Tanzania ilishuka thamani kwa style ile ya ruksa, maana huwezi ruhusu vitu kuja nchini vikaiacha rafu ya nchi salama haitawezekani. Kwa hivyo tutafurahi kuja kwa vitu lakini sio tatizo la kuondoa umasikini au kuleta maendeleo nchini.
Benjamin Mkapa, alichokifaya mkapa katika utawala wake ndo kitu ambacho mwinyi alitakiwa afaye wakati ule, lakini kosa la mkapa ni moja kuua viwanda vya ndani, mkapa alitakiwa afanye ubinafisishaji kwa usawa, unabinafisisha lakini serikali au wananchi wanakuwa na hisa/maamuzi makubwa zaidi, kila shirika unalobinafisisha unahakikisha over 50% za hisa zinakuwa chini ya serikali . Pia alitakiwa aendeleze kulinda viwanda vya ndani, je angelinda viwanda vipi? jibu hakuna, je alitakiwa amlaumu mwinyi kwa kutokuwa na viwanda jibu Hapana, yeye angeanza moja kwa moja kuja na sera ya kilimo na viwanda tukaanzia pale leo hii tungekuwa mbali.
Pia Kuna tatizo katika ubinafisishaji mwanya wa wizi unaongezeka sana hili swala likaibuka na likamshinda Mkapa, kwa nini? hakuwa na sera nzuri ya kupambana rushwa. Lakini kwa upande wa huduma walau alijitahidi, barabara zikajengwa, mashule mengi yakafunguliwa hata ya kata, mikopo vyuoni, na akajenga taasisi japo si imara yaani kwa ufupi mkapa katupeleka western zaidi na kuzika issue za ujamaa.
Swali ni moja tu hapa, je Tanzania itaendelea kwa kutegemea uagizaji wa bidhaa kutoka nje? jibu Haitawezekana na nikupoteza muda kuwaza hivyo.
Kwa maelezo hapo juu, mtajua sasa ni dhama ipi ilikuwa na lengo la kuondoa umasikini Tanzania japo kwa maumivu, pia Tanzania tunatakiwa kujua hatutakuja kuendelea bila kukubali kuumia au kufanya kazi kwa bidii aua kuthamini vitu vyetu vya ndani, tunaweza tukawa na njia za haraka haraka za mikato lakini tujue maendeleo ni kitu kingine hakihitaji comparison ya uislam wala ukristo, ccm wala chadema kina hitaji nidhamu kupanga na kufanya.