Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Akiwa waziri wa mambo ya ndani alijiuzulu baada ya kupata taarifa kuwa polisi wameua raia huko shinyanga, akaenda kukaa uswahilini huko Tandika, alimsamehe mtu ambae alimvamia na kumpiga mtama, haya mambo niliona ni jinsi gani tulikua na raisi mcha mungu na asiependa makuu/sifa, alikua na kauli, nahau au misemo ya kiswahili yenye kufurahisha kuelimisha na kukutafakarisha, mfano "Dereva mzuri hawezi acha usukani kumpiga mbu anaemn'gata" "Biashara ni kuuziana na kununuliana" Gonjwa hili limekaa mahali ambapo sote twapataka" "mali bila daftari hupotea bila habari" na mingine mingi ndio maana mpaka leo tunamuona na upole wake usio na makeke wala kiburi kwa binadamu wenzake, hudhuria sherehe au hafla yoyote ukitaja jina la Mzee Mwinyi (mzee wa ruksa) utaona jinsi watu wanavyomshangilia hii ni kuonesha jinsi watu walivokua wanamkubali na hana kashfa yoyote ile ya matumizi mabaya ya madaraka au kupora mali ya umma na kujilimbikizia mali watanzania tutamkumbuka sana huyu mzee, Mwenyezi Mungu amjalie maisha marefu
 
Ngoja Tuanze na mazuri yako, maana hata wewe ukifa ndugu zako na watu mbali mbali watakumwagia sifa kedekede. Ngoja Tuanze na wewe then tuje kwa mimi pamoja na Mwinyi. Maana unaweza ukafa wewe au Mimi kabla ya Mwinyi..... Tuanze na wewe Mkuu.
Ndo umeandika nini hapa we pungua.ni?
 


1. Alifungua uchumi wa soko huria (economic liberalisation); serikali ikaanza kujitoa kwenye uchuuzi; nchi ikatoka kwenye ujima kuelekea
maendeleo ya kisasa.
2: Alisimamia mabadiliko ya kutoka mfumo wa chama kimoja kwenda vyama vingi bila hiana wala vitisho vya dola.
3: Hakuwahi kuangaishwa sana na "kelele za mlango"; kutafuta wachawi na wanaompinga.
4: Ni mtu muungwana sana, mnyenyekevu ambaye alijaribiwa sana lakini akabakia kama binadamu, akasamehe na kusahau; Hana visasi wala mtimanyongo
5: Hakulewa madaraka na kujiona kama Mungu mtu.
6: Hata hivyo upole wake na kauli mbiu ya "kila kitu Ruksa" vilipandikiza mbegu za rushwa na ufisadi unaolitikisa taifa letu leo!
Pamoja na mapungufu yake ya kibinadamu anabaki kuwa mmoja wa Marais wetu kipenzi cha watu wengi, na ndio maana kila anapofika kwenye hadhara yoyote utasikia nderemo na kelele za Mzee Ruksa, Mzee Ruksa, kwa sababu ya tabia yake ya kupenda watu, kutolewa madaraka, na kutojiona kama "ameinunua nchi"; no wonder ukimuona leo utadhani ni mtu wa umri wa kati kumbe keshagonga 90! Anafarijika na kupata thawabu kutokana na upendo anaouona miongoni mwa wananchi wake
 
mbona wapo wengi ujahoji jombi !kama mwalimu, karume ,mkapa ,kikwete ,muheshimiwa magu ! au nao sio watu jombi ?
Mkuu mimi nimeanza na huyu nafahamu wapo wengi hata wew unaweza ukaanzisha uzi kwa wengine maana wapo wengi, wapo akina malecela, warioba, salim.. wapo wengi mno
 
Zuri la Mwinyi lililo onekana mpaka leo ni kuwa na wake wawili na hili tunalifanyia kazi, hakuna lingine lililo onekana.
 
yapo mengi ila haya yanabeba yooote yaliyobakia.
 
Pia enzi hizo za kulikuwa na maduka ya kaya.

Unga wa sembe wa njano.

Ukimuona mtu amevaa raba nzuri(raba mtoni) ujue ana ndugu ulaya au bahari.
Mtaani kwetu kulikuwa nyumba moja tu ina TV kwa dr Mhando.

Dah!!! Hata kandambili ilikuwa shida.
Tumevaa sana katambuga za matairi ya gari.

Yale maisha yalikuwa si mchezo.
 
Nashukuru leo brother unamwaga Nondo zakutosha... tujiulize kwanini KAWAWA anapondwa na kwa nini MWINYI ANAPONDWA NAKIKWETE AMEPONDWA LAKINI WENGINE WANATUKUZWA KWA KUONEKANA NI WAZURI KIUTENDA..
Umeshataja majina, nenda upande wa pili mwenyewe halafu turudi kwenye mada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…