Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Licha ya ucha Mungu pia ni Baba na Babu bora kabisa wa familia yake, watoto na wajukuu zake wengi wananidhamu na ubinadamu kama yeye mwenyewe.
Mkuu nakuunga mkono kabisa sample yangu kuna mjuu wake binti mdogo tu anaitwa Sitti Mwinyi naweza kukapa nidhamu A.
Heshima kwa wakubwa iko vizuri sana hakuna nyodo kabisa, heshima to the family kwa kweli.
 
Hali ilikuwa mbaya kupita maelezo
nchi nzima watu wanavaa katambuga
sabuni za magadi na majani ya mpapai..
mahindi ya msaada kutoka marekani ya njano
yaliitwa mahindi ya Yanga....
ukikutwa na sigara box zima unakamatwa kwa uhujumu uchumi
Unatukumbusha mbali sana tena sana, watu tumetoka mbali, Mzee Mwinyi ndie aliyefanya watanzania wengi wajue kama tv. Nchi kabla yake iliongozwa kidikteta hakuna aliyethubutu kusema lolote baya kwa Mwalimu.
 
Tazama hapa uadilifu na ucha mungu wa mzee wetu kipenzi
Tazama maneno yake kwenye barua hii ya kujiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani mwaka 1977

Alli hassan mwinyi.
 
Sidhani kama anaweza kuja Rais tena mwenye subra na uvumilivu, huruma, mpole na mwenye mahaba ya dhati na watu wake kama Ally Hassan Mwinyi.
 
Mh.Ali Hassan Mwinyi kweli watu walinemeeka kuanzia wakulima, wafanyakazi,wafanyabiashara nk....Kipindi cha Mwinyi babu yangu aliweza kununua Bedford 2 na Mzee wangu kununua Land Rover na Suzuki Samurai...
Mwinyi hakua na chuki na watu wasiokubaliana nae kabisa ...Ila kuna hisia na mawazo kua Tanzania inapokua na kiongozi muislam mambo yanaenda vizuri kuliko inapokua na kiongozi mkristu...Je kuna ukweli au ni porojo tu
 
Umenifurahisha sentensi yako ya kwanza
 
Mkuu kwani hayo ayasemayo THE BOSS kuhusu MZEE RUKSA ni ya uongo??

RUKSA ALIITOA HII NCHI KWENYE TONGOTONGO NA GIZA KALI..
Kabisa mengi kamaliza the Boss. Nakumbuka mwaka 1984 watoto wa shule zote (msingi na sekondari) ambao sare zao zimechanika waliruhusiwa kutumia kitambaa cha madurufu (sanda) kushona sare za shule maana ndio kitambaa pekee kilichopatikana kwa wengi madukani. Mzee Mwinyi alipoingia madarakani akasema "ruksa" kuingia bidhaa nchini.
 
1. ALIFUATA TORATI YA MUSA NA KUWANYONGA WOTE WALIOHUKUMIWA KIFO NA MAHAKAMA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA TANZANIA BILA MZAHA WALA UPENDELEO AKIWEMO KANALI MMOJA TOKA TABORA NAMPENDA SANA KWA HILO
2. ALIWABEBA SANA WAFANYABIASHARA KIASI KWAMBA AJIRA IKAONEKANA NI UPUUZI NA WENGI WALIACHA KAZI SERIKALINI KWAKUWA MISHAHARA ILIKUWA HAIPATIKANI MPAKA WAFANYABIASHARA WAPELEKE FEDHA BANK NDIPO MFANYAKAZI APATE MSHAHARA NI KATIKA KIPINDI CHAKE ALINISABABISHIA NIACHA KUSOMA BAADA YA KUONA KUAJIRIWA HAKULIPI KAMA KUFANYA BIASHARA
3. ALIMDEKEZA SANA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU PROF. KIGHOMA ALI MALIMA AKAJENGA MSIKITI WIZARA YA FEDHA.
4. NI KATIKA KIPINDI WAISLAM WALITAKA TANZANIA IONGOZWE KIDINI NA MKAKATI HUO ULIONGOZWA NA MAREHEMU SHEIKH YAHYA HUSSEIN KWA KUANZISHA BALKUTA NA KUANZA KUVUNJA MABUCHA YA NGURUWE NA NI KIPINDI HICHO NYAMA YA NGURUWE ILIITWA KWA UTANI "YAHYA" AU MBUZI KATOLIKI
5. NI KATIKA UTAWALA WA MWINYI SERIKALI ILIKUWA HAIKUSANYI KODI NA WAFANYABIASHARA WALIKUWA NA NGUVU YA KUFANYA LOLOTE NA IKULU PALIKUWA PANAINGILIKA KIRAHISI SANA HATA UKIWA NA SHIDA YA ADA YA SHULE ULIRUHUSIWA KUMUONA RAIS NA UKIHITAJI KUCHEZA BAO NA PRESIDAA UNAOMBA NA UNAINGIA KAMA ALIVYOFANYA MWENYEKITI WA YANGA NA MBUNGE WA KILOMBERO MAREHEMU ABBAS GULAMALI. NAISHIA HAPO.
 
Kiukweli kipindi cha Mzee RUKSA" maisha yalikuwa mazuri,kwakuwa pesa ilikuwa inapatikana kwa urahisi sana pia Huduma za kijamii zilikuwa si haba.Tuliosoma kipindi kile tulikuwa na uwezo wa kujinunulia japo madftari kwani yaliuzwa senti tano kwa yale ya mistari mikubwa na yale ya mistari midogo yani ya mwandiko yaliuzwa shilingi moja.
 
Mkuu awamu ya kwanza Mwinyi alimsikiliza Nyerere kwa kuwa alishika rungu la uenyekiti Ccm hivyo aliogopa kumkuta ya Aboud Jumbe.Mwishoni mwa awamu ya kwanza na awamu ya pili mambo yalibadilika baada ya Mwinyi kuwa na full authirization ya nchi na chama na hapo ndipo akaua azimio la Arusha kupitia Azimio la Zanzibar na kubadilisha mfumo wa nchi kiuchumi na kisiasa kimapana zaidi kiasi Nyerere akaanza kuona Mwinyi amekengeuka na kuamua kuandika kitabu kumshutumu kuua Azimio la Arusha na kwamba anashauriwa na mkewe.Ajenda ya vyama vingi ilikuwa ni ya Mwinyi ndio maana akaunda tume ambayo ilionyesha waTz wengi hawakutaka kutokana na hofu badala yake wakasuggest vitu ambavyo vilionekana kwamba vinawezekana tu iwapo kutakuwa na vyama vingi.Kwa kupitia hilo Mwinyi ndio akaruhusu vyama vingi ingawa pia kwa wakati huo Nyerere hakuwa na ubishi nalo.
 
Kifupi ni kwamba rais wetu WA Sasa aige mengi kutoka Kwa MWINYI
Hiyo ni mbingu na ardhi!!! Mzee Mwinyi hakuwa mtu wa visasi, alikua mtu anaeshaurika na kuchukua hatua baada ya tafakuri ya kutosha, alitamani wananchi wake waishi kama malaika hakupenda watu wawe maskini aliruhusu mijadala ya kumkosoa ndio maana alisema "dereva mzuri haachi usukani ili kumpiga mbu anaemn'gata"
 
Ahsante sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…