Alikuwa anamsikiliza Nyerere weeeeee, hambishii, akitoka hapo anafanya anavyoona yeye inafaa!
Enzi zake vijana wakaanza kwenda Dubai kuleta mali
Aliamua makusudi kutokusanya kodi kutoka kwa Makabwela ili kuwajengea watu uwezo wa kifedha, ili baadae wapatikane watu wa kuwatoza kodi..
Alilichinjilia mbali Azimio la Kimasikini lile Azimio la Arusha, Wewe umewahi kuona wapi Azimio linazuia watu kumiliki hata nyumba ya kupangisha eti kisa wewe ni Mwenyekiti wa kijiji.
Wakati anaondoka madarakani almost kila mtu akawa ana TV, watu tumeangalia World Cup mwaka 1994 ITV, tumeangalia Kombe la Mataifa huru ya Afrika yaliyofanyika Tunisia mwaka 1994 Live kila mtu na kideo chake nyumbani!
Pesa ilikuwa inapatikana, Vijana wakaanza kuangusha majumba ya hatari Mbezi, Tabata, Sinza
Aliandikwa vibaya sana na Magazeti kama RAI ya Jenerali Ulimwengu lakini hukusikia anayafungia!
Long live mzee Ruksa, Uko mioyoni mwetu forever!