Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Hekima ya kutotaka bifu na Magu muhimu sana kwa sasa hongera zake
 
Good!
 
Mwinyi na Magufuli wote wamekua marais kwa bahati.

Mwinyi walikubaliana na nyerere kwamba mwinyi kwemye kikao akatae ili nyerere aendelee.. kumbe mwingi baada ya kumwambie mkewe.. akaambiwa kama atakataa asirudi nyumbani..

Mwimyi baada ya kuulizwa akajibu nipo tayari na nashukuru kwa fursa na ndio mwanzo wa nyerere kusema mtu unashauriwa mkeo kitandani .

Wote hawakuwa na mpango nini watalifanyia taifa hili.
 

Hiyo Crisis ilisababishwa na Vita ya Kagera 1978/79 (katika kuweka kumbukumbu sawa though nilikuwa mdogo lakini nakumbuka unga wa Dona ulivyokuwa "dili"😳😳😳)
 
Mimi kama mfanyakazi nitakuwa wa mwisho kumpongeza Rais Mwinyi maana katika utawala wake ndo kipindi wafanyakazi walidharauliwa hata na wauza machungwa barabarani, kilikuwa kipindi kigumu sana kwa kundi la wafanyakazi wa umma. Bila Rais Mkapa kubadilisha mambo sijui nchi hii kama ingekuwepo hadi leo. Maana ni kipimdi ambacho serikali ilikuwa dhaifu sana haikuweza kabisa kukusanya kodi nakumbuka hadi Nyerere alisema serikali dhaifu huwa zinaacha kukusanya kodi kwa wafanya biashara na kufukuzana na machinga barabarani. Sasa Kiongozi aliyeomgoza serikali dhaifu kiasi kile labda akumbukwe kwa hiyo sifa ya kuwa na serikali dhaifu sana.
 
Kuna dhahabu ilikamatwa airport ikimuhusu huyu mzee!! Mrema anakumbuka vizuri!
Legacy ya wizi ndiyo aliiacha pamoja na matangazo ya kondomu. (kelbu)
 
Legacy yake ni vile vibao alicharazwa msikitini! Yule jamaa angempiga ngumi kabisa!
 
Shairi zuri zana hili ukioimbaa
 
uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi mwaka 83 kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa mzee mmoja kutoka zanzibar anaitwa mzee natepe kushika uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Natepe alipoingia tu officen alimtaka waziri aliemtangulia kutoka katika nyumba ya waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama waziri.

Ilikuwa shida kidogo maana waziri alieondoka bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Natepe.

Ikampasa mzee mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake wala sio mali ya serekali.

Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya serekali kweli mzee mwinyi akaviacha akaondoka.

Baada ya miezi kadhaa tu mzee mwinyi akateuliwa kuwa Rais zanzibar Natepe wakati ana jifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza na kumuomba radhi kwa aliyomfanyia kabla ya kufikiria njia mzee mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa JMT.

Hapa sasa Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za JMT kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea mzee mwinyi.

Mzee mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua baraza la mawaziri akamteua tena Natepe kuwa waziri pale pale mambo ya ndani.

Siku ya kumuapisha akamwambia Natepe sio kwamba nakupenda sana hapana ila napenda kazi yako unavyofanya endelea kufanya kazi.

Siku moja mzee mwinyi yupo ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu mh Rais akashtuka mbona sijaagiza kitu mie??

Ndipo akaambiwa umetoka kwa natepe mzee mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.

Hapa kuna masomo makubwa ma tatu vema viongozi wetu wa sasa wakajipambanua kwayo ili tuende kwa weledi na umakini sana.
 
Hongera kwa jua yaliyomo vyumban kwa watu
 
Mzee wa Ruksa...

Ana busara sana na haendekezi uswahili... hii imepelekea mpaka familia yake kua ni wale watu wenye kufuata maadilii...


Cc: mahondaw
 
Kweli mkuu, mi nakumbuka nikiwa mdogo miaka hiyo(nilikulia Kariakoo,Tandamti na Jangwani,au tuseme, Tandamti na Msimbazi),nikimwona mtoto kavaa kandambili pea moja(yaani zinazofanana), nashtuka! nahisi kwao matajiri! maana kwetu ya kushoto azam,kulia yanga,au kushoto simba, kulia ..... yaani ni kawaida kuvaa kimasikini-masikini.

Nakumbuka kisa kingine nilienda kwa kucheza kwa jirani zetu, mida ya mchana ilipofika, ukaletwa ugali una rangi nzuri ya manjano kama jezi ya timu yetu ya Taifa...kwa nilikatazwa kula kwa majirani,niliporudi nyumbani nililalamika sana kuwa wale mbona ugali wao mzuri una rangi,na sisi wa kwetu mweupe!

Nakumbuka kuna mjomba wangu alifika kutoka kijijini, baada ya kupiga naye stori,jioni ilipofika tulimsindikiza kwa mjumbe wa nyumba kumi kumtambulisha (Mareh. Mzee Chaurembo- ILWIR).
Pia nimewahi kutumwa kupanga foleni kwenye "duka la kaya" kwa mahitaji kama sukari na unga.

Kwa kweli nami ni mmoja wa aliyeufurahia utawala mpya wa Rais Mwinyi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…