Legacy zinavyopotea haraka, nahisi huruma

Legacy zinavyopotea haraka, nahisi huruma

goukun wadey

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2020
Posts
241
Reaction score
284
Nahisi huruma sana jinsi hii kitu inayolazimishwa legacy ya Magufuli kwa sababu, kwanza ni nature ya Mwanamke kuwa na Huruma, pili asili ya mtu na makuzi yake.

Ninapojaribu kuwaza jinsi ambavyo itakuwa ngumu kuenzi mambo ya Mtangulizi wa Samia! Ni kwa hulka za hawa wawili kutofautiana sana. Hivyo watanzania watakuwa ama wakumbuke kuendelea kunzi ukatili katikati ya mtu mwenye huruma, au waenzi ukatili ulio kinyume na mtawala wa sasa ambae kwa hulka ya asili yake na makuzi yake sio mtu KATILI. Ukijaribu kurejea hotuba za mwanzo kabisa za Samia unakutana na maneno 'sitaki fedha ya dhulma'.

Viongozi tuwe kitu kimoja, fungueni vyombo vya habari, na mengine mfano wa hayo utajua kwamba hii kitu inayohimizwa sana na kambi ya D7 (legacy) itakuwa ngumu kudumu kwa sababu Magu atakumbukwa sana kwa ukatili kuliko mambo mengine kwa sababu ya aina MRITHI wake.

Hivyo kambi D7 tuwe wavumilivu
 
Hivyo watanzania watakuwa ama wakumbuke kuendelea kunzi ukatili katikati ya mtu mwenye huruma, au waenzi ukatili ulio kinyume na mtawala wa sasa ambae kwa hulka ya asili yake na makuzi yake sio mtu KATILI. Ukijaribu kurejea hotuba za mwanzo kabisa za Samia unakutana na maneno 'sitaki fedha ya dhulma'.
You Nailed it "UKATILI" visa vis "HURUMA" Mwendazake and SASHA respectively.
 
Kwani Meko alikua ni nani hasa yeye? Mbona mnazuia watu wasiteme nyongo zao za miaka 5? Alikua ni Rais wa hovyo kuwahi kuitawala Tanzania...

Meko ashakufa hivyo tuachane na habari zake, nchi iko mikononi mwa Mama anaiendeleza na kufuta upuuzi wote uliowekwa na mtangulizi wake..
 
Na Kwa nini kila anaemfagilia Hayati aonekane si binadamu tena miongoni mwa jamii ndoogo ya watu waliochanganyika wema 2% na wauza madawa, wenye vyetu feki, majizi na mafisadi pamoja na wazembe 14% tu Kati ya watu wema ujumla wa 84% waliopendezwa na mfumo na utendaji kazi wake?

Ni ujinga na upumbavu kudhani Kwamba, watu hao walioamua kuwa upande wake hawastahili kufanya hivyo
 
Back
Top Bottom