February 2, 2020
Mh. Lema atoa ushauri kwa idara za serikali kuhusu usalama
Mh. Lema mbunge wa CHADEMA na waziri kivuli wa Mambo ya Ndani kambi ya upinzani, atoa ushauri kwa vyombo vya usalama kama Jeshi la Polisi, Idara ya Zimamoto na Uokoaji juu ya kujipanga popote kunapokuwa na mikusanyiko ya kiimani, kisiasa na kijamii.
Amekosoa vyombo vya usalama kujikita zaidi kukabiliana na changamoto za upinzani na kuzembea maeneo mengine ambayo pia yanahitaji mipango thabiti ya usalama.
Vilevile ametaka vyombo hivyo vya usalama kupewa mafunzo ya weledi jinsi ya kukusanya taarifa za intelejensia na kupewa mafunzo ya kudhibiti mikusanyiko mikubwa ya watu ili maafa yasitokee.
Source : ABC Habari