Pre GE2025 Lema aomba radhi kwa kauli aliyotoa dhidi ya mke wa Nape lakini ashikilia msimamo wake juu ya kauli ya Nape

Pre GE2025 Lema aomba radhi kwa kauli aliyotoa dhidi ya mke wa Nape lakini ashikilia msimamo wake juu ya kauli ya Nape

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Ameandika Lema katika mtandao wa X:

"Jana wakati nakemea kauli yako katika mkutano wa hadhara Murriet Arusha dhidi ya kauli yako na mipango yenu ya KIPUMBAVU juu ya wizi na uporaji wa kura katika chaguzi zinazokuja, nilijikuta natoa mfano mkali ambao umemgusa bila shaka Shemeji yangu mpendwa (Mke wako).

Kuona kauli yake dhidi ya Nape soma: Lema: Nape mpumbavu wewe sisi tunaweza kumuiba mkeo na kukaa nae chumbani kwetu

"Namheshimu sana Mke wako, tafadhali shemeji yangu aniwie radhi, naomba nipelekee salamu hizi kwake. Hata hivyo bado nasisitiza kuwa kauli yako ni hatari kwa usalama wa Nchi na ya KIPUMBAVU na wewe ni Mtu mwenye KIBURI sana."

Pia soma: Nape: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!

1721225732691.png
 
Tofauti pekee ya Lema na Nape ni vyama vya kisiasa walivyokuwepo. Kinyume na hapo ni kama pipa na mfuniko tu, wote mabwaku bwaku.
 
Ameandika Lema katika mtandao wa X:

Jana wakati nakemea kauli yako ktk mkutano wa hadhara Murriet Arusha dhidi ya kauli yako na mipango yenu ya KIPUMBAVU juu ya wizi na uporaji wa kura ktk chaguzi zinazokuja, nilijikuta natoa mfano mkali ambao umemgusa bila shaka Shemeji yangu mpendwa (Mke wako). Namheshimu sana Mke wako,tafadhali shemeji yangu aniwie radhi,naomba nipelekee salamu hizi kwake.Hata hivyo bado nasisitiza kuwa kauli yako ni hatari kwa usalama wa Nchi na ya KIPUMBAVU na wewe ni Mtu mwenye KIBURI sana.
Ni mpumbavu tu
 
Back
Top Bottom