Uchaguzi 2020 Lema ashtushwa na mpango wa msimamizi wa uchaguzi Arusha kubandika wapiga kura hewa laki 1

Uchaguzi 2020 Lema ashtushwa na mpango wa msimamizi wa uchaguzi Arusha kubandika wapiga kura hewa laki 1

Waziri2025

Senior Member
Joined
Sep 2, 2019
Posts
148
Reaction score
379
Akiongea na Vyombo Vya Habari katika Ofisi za jiji la Arusha wakati akiwasilisha malalamiko yake kwa Mkurugenzi msaidizi wa uchaguzi dkt John Pima ,Mgombea Ubunge wa jimbo la Arusha Mjini chadema,Godbless Lema amedai kushtukia mpango uliosukwa wa kuongeza majina hewa ili kukipa ushindi Chama cha mapinduzi.

Akiongea kwa uchungu huku akilengwalengwa na machozi ,Lema amesema awali wapiga kura kwenye daftari la kudumu jimbo la Arusha mjini walikuwa zaidi ya laki 240 lakini Jana wameshangaa kuona kwenye daftari hilo kuna wapiga kura zaidi ya laki 370 ikiwa ni ongezeko la wapiga kura hewa zaidi ya 100 .

Lema amesema baada ya kumuuliza dkt. Pima ameshindwa kutoa ufafanuzi badala yake aliwatuliza viongozi wa chadema na kuwataka wafike Ofisini kwake ili atoe ufafanuzi.

Hata hivyo Lema amesema Chama chake kimejipanga kuandika barua ya malalamiko kwa Mkurugenzi wa uchaguzi NEC ,dkt Wilson Mahera kupeleka kilio chao

Amesema ameshutushwa pia na hatua ya Mgombea wa ccm,Mrisho Gambo kwenda kuomba kura kwa wanafunzi wa sekondari ambao alidai ndio wametayatishwa kupiga kura siku ya uchaguzi jambo ambalo aliwaonya Wazazi wao kutowaachia watoto wao waliochini ya miaka 18 kushiriki mchezo huo mchafu wakati hawakujiandikisha kuwa wapiga kura.

Halikadhalika amesema kuwa ameshangaa katika Ofisi ya Mkurugenzi kumkuta mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi na DSO wakichambua fomu za mawakala jambo ambalo mkuu wa wilaya hahusiki kabisa na suala la uchaguzi na kudai kuwa kuna mpango wa maksudi wa kuhujumu mawakala wao.

Hata hivyo waandishi wa Habari waliofurika katika Ofisi za jiji la Arusha kutaka kupata ufafanuzi wa tuhuma hizo kwa dkt Pima msimamizi msaidizi wa uchaguzi, alikataa kutolea ufafanuzi jambo hilo huku akiahidi kuita wanahabari kwa muda wake.

"Nitawaita wakati mwingime nitaonga na nyingi si jambo hili tu nitawaeleza na mengine yanayohusi uchaguzi" alisema huku akiingia Ofisini kwake.
IMG_20201021_154534.jpg
 
...Tume iwakemee watendaji wa mikoa, wilaya wanaojaribu kuvuruga uchaguzi.

Sio kuwakemea mtu mkuu, bali ni kuchukua tu sheria mkononi. Tume ndio wanaotumika na ccm kunajisi uchaguzi. Na haya ni maagizo ya rais ili kulazimisha ionekane anakubalika. Machafuko tu ndio suluhu ya hizi tabia za viongozi wa kiafrika.
 
Na kwann wameongeza laki moja tu, wangefanya angalau 500K, cha msingi ili lichama lifutwe tu tupate upinzani kutoka vyama vingine ikiwezekana waungane
 
Ha ha ha lema amepata kihoro, kwa alichokiona Mo Town na Hai leo. Kesho atazimia kabisa. Hakuna kitu kinauma kama kujiandaa kula, halafu unyimwe chakula tena mbele ya hadhara. Kafanya kampeni weee, Magufuli anakuja kutibua kila kitu. Magufuli kesho kanyajia palepale.
 
Back
Top Bottom