Lema kurudishiwa ubunge: Je nini kifanyike kwa majaji waliofuta ubunge wake

Lema kurudishiwa ubunge: Je nini kifanyike kwa majaji waliofuta ubunge wake

Joined
Mar 5, 2012
Posts
90
Reaction score
23
TUJIFUNZE YAFUATAYO:

  1. Kumbe ni kweli watu wengi wanaonewa
  2. Je inapotokea majaji wametumia vibaya taaaluma zao, je nini kifanyike? Wana-Arusha mjini wamekosa mwakilishi kwa kipindi kirefu sababu tu ya majaji ambao ama hawajui kuchambua sheria au walihongwa au wana sababu ambazo wanajua wenyewe.
  3. Fedha nyingi zimetumika na Lema, chama chake(chetu),pamoja na fedha kuendesha kesi ambayo mwisho wake tunaona ilikuwa ni makosa
  4. Muda wa-Tanzania umetumika vibaya, kwani ungeweza kutumika kujadili mambo mengine. Magzaeti yamekuwa yakiandika hili, wakati kurasa hizo zingeweza kutumika kutoa habari nyingine.
  5. Narudia tena, kama ilivyo kwenye TUME nyingi zinaundwa, mwishowe tunapata report feki, je nini kifanyike inapoonekana fedha za wa-Tz zinatumika vibaya kupitisha maamuzi ya wadhulumaji wa raslimali za nchi

PENGINE: KATIBA MPYA- Itoe suluhisho,mtu yeyote, au chombo chochote kikitumia vibaya mamlaka yake(kama hawa majaji)-wapelekwe mahakamani na ikithibitika kuwa walifanya kazi nje ya weledi wataaluma zao- WAFUNGWE maisha: HII ITASAIDIA.


TUJADILI
 
I liked the reasoning of the Court of Appeal on what in law we call "locus standi". The Court of Appeal satisfied itself snd has ruled out that election petition is not a public interest litigation though it has public importance. The Respondents,Musa Mkanga et al had no locus standi to file the petition against Godbless Lema. The Court of Appeal also wondered how Mujulizi accepted to admit the docs which were not filed in Court using a proper manner.Lema was therefore right to refuse Mujulizi from presiding over his matter since the judges conducts were enough to make any reasonable person to come to the conclusion that justice would not have been done had he presided over Lema's matter.

The battle continues
 
Yah ! Ni kweli tunahitaji kujiuliza kitu cha kufanya ili kutokomeza haya mambo ya vyombo vya sheria au hata vyombo vya usalama kujidhalilisha kwa kupewa maagizo na wanasiasa , tunapoteza muda mwingi sana kijinga mno !
 
Nimeamini Lema ana Mungu.Watashindana lakini hawatashinda!!!
 
tuwafungulie kesi majaji makanjanja ambao wamesababisha pesa za watz kutumika vibaya. Kweli majaji hawana elimu ya kutosha pumbafu sana
 
majaji na mahakimu wana judicial immunity
ya kutochukuliwa hatua wanapotoa maamuzi kama hawajakiuka maadili
hiyo iko worldwide,ndio mana kuna haki ya rufaa kama hujaridhika na hukumu au mwenendo wa kesi
 
Yah ! Ni kweli tunahitaji kujiuliza kitu cha kufanya ili kutokomeza haya mambo ya vyombo vya sheria au hata vyombo vya usalama kujidhalilisha kwa kupewa maagizo na wanasiasa , tunapoteza muda mwingi sana kijinga mno !
Huwezi kuwafanya chochote hao majaji coz sharia inakukataza kuwafanya chochote na wana immunity.
 
hongeraaaaaaaaaaaaaaaaa sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kamanda lema penye ukweli uongo hujitenga Mungu yuko nasi daima
 
Wakati nasari anapata ubunge alisema maneno fulani nami nanukuu ...'''' TULIANZA NA MUNGU ...TUMEMALIZA NA MUNGU....''' Kwa maneno hayo ni kwamba Lema alianza na Mungu na kumaliza na Mungu...
 
Hapo ni Mungu tu wakuu kafanya,JK alifurahia sana kuvuliwa ubunge kwa lema mpaka akasema amani Arusha imerudi
 
Bado wanahangaika na fuko lao la TZS 150,000,000

Hapo hizo lazima wamepeleka mgawo mkubwa hadi kwa Kova na kwa Msangi ambaye amepewa kazi ya kuchunguza,Msangi na KOVA NI MAHARAMIA HATARI NA WOTE WALIFANYA KAZI ARUSHA WAKATI WA KAMANDA TIBAIGANA NA MAJAMBAZI WAKALI KAMA MASAWE,MINJA,CHONJO,MJUSI.HAPO sioni taarifa sahihi kutoka kwa polisi Kova huyo ni kamanda tu wa majambazi.Kwanza tumuombe taarifa ya Msangi ya kupigwa Ulimboka iko wapi?,kama siyo kuzuga wananchi?
 
Makamanda wetu hongera sana tena sana. Mwendo ni huo hadi 2015! Mungu awabariki sana na awarudishie mara elfu muda wenu mliopotezewa!
 
...Kwamba wanajua au kutokujua, majaji hao wanaendeleza tu mfumo wa udhalimu uliokuwepo zama za manabii kama alivyoandika nabii huyu Habakuki katika Biblia....
"Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea…. Kwa sababu hiyo SHERIA IMELEGEA, wala HUKUMU haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa sababu hiyo HUKUMU ikipatikana IMEPOTOKA!!". – (Habakuki 1:4)

Kama alivyolalama huyu bwana, naamini uchungu wa kupewa hukumu iliyopotoka hauvumiliki...(unbearable)..
Whilst am congratulating Bwana Lema for the revised judgement, lakini hao majaji hata kama sheria haiwezi ku-take its course for them....they will in their turn face the judgement from the most High God!!
Just trying to think loud....
 
Back
Top Bottom