Halaiser
JF-Expert Member
- Apr 3, 2014
- 4,230
- 6,653
Mkuu hii haina tofauti na mzazi anaenunua gari na kuliegesha nyuma ya nyumba yake tena ni ya tembe. Wakati huo watoto wanaishi kwa mlo mmoja tena kwa jubahatisha. Shule wanatembea peku. Eti nae baba yule bila huruma a awaambia wale watoto nimeshawaandalia gari mara mtakapomaliza elimu yenu ya msingi basi sekondari hamtatembea tena kwa miguu bali gari hili. Wale watoto pamoja na upeo wao mdogo wanaona wazi baba yao kachanganyikiwa kwani kwa mazingira yale hawana uhakika wa kumaliza elimu ya msingi wakiwa salama na wenye afya njema.Wanasema sio kama anavyolipa Magufuli cash,sijui wao wangelipa kwa mawe
Vipaumbele vya awamu ya tano ndiyo tatizo. Kila jambo na wakati wake. Hebu fikiria kama wa geamua kufufua kiwanda cha General Tyre kwajili ya uzalishaji wa matairi ya magari ni ajira kiasi gani ingezalishwa na faida kiasi gani tena kwa soko la ndani tu ingepatikana?? Je faida ile isingetosha kununua ndege?? Tuwe tunatafakari kabla ya kutenda.