Lema: Narudi Tanzania

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Godbless Lema asema anafikiria kurudi nyumbani Tanzania,

Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye alikimbilia ughaibuni kwa madai ya wasiwasi wa usalama wake mara baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 anafikiria kurudi nchini Tanzania.

Baada ya kifo cha Rais Magufuli Lema anatarajia kuona uongozi wa Rais Samia ukirekebisha na kutafuta maridhiano ya taifa zima.

‘’Nataka kurudi nyumbani hata leo, nyumbani ni nyumbani tu, wakati nakimbia nyumbani nilishuhudia uzoefu mbaya mimi na familia yangu’’, alisema

Lema ameeleza kuwa mabadiliko ya mifumo ya kiutawala ikiwemo viongozi watakaojali haki ni sura itakayorejesha imani ya kwamba sasa maisha yako salama.

‘’Nitarudi nyumbani mapema sana kuendelea na mapambano. Uwepo wetu huku hauna maana ya kwamba tumekuja kula bata, hakuna maisha yoyote, mtu anaweza akakimbia nyumbani kwao ambako amejijenga vizuri.’’alisisitiza

Hata hivyo Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ilitupilia mbali madai hayo ya upinzani na kusema hayo ni maigizo ya upinzani.

‘’Tanzania ni nchi inayoheshimu utawala wa sheria.’’alisema msemaji wa serikali Dokta Hassan Abbas.

Samia Suluhu Hassan ameapishwa leo jijini Dar es salaam kuongoza awamu ya sita ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kifo cha mtangulizi wake John Pombe Magufuli.
 
Rejea nyumbani Lema, hapa ndio kwenu unapotakiwa kuishi kwa amani bila kutishwa na mtu.
Rudi utumikie nchi yako.

Kuna watu hudhani hii nchi ni yao peke yao, hii nchi ni yetu sote maana tumezaliwa hapa wala hatukuomba uraia kwa kujaza makaratasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…