Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema amesema atamshauri Mwenyekiti mpya wa Chama hicho Taifa, Tundu Lissu kuanda mkakati wa kumuaga rasmi na kutambua mchango wa Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe ambapo pamoja na zawadi nyingine amesema wanaweza kumtafutia Land Cruiser 200.
Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) Lema ameandika “Mwenyekiti Msatafu na Mjumbe wa Kamati Kuu Mh. Freeman Mbowe alifanya kazi kubwa za ujenzi wa Chama na mageuzi, nitamshauri Mwenyekiti Lissu kuwa ni jambo la maana kuaanda mkakati maalumu wa kuheshimu commitment yake na kumuaga vizuri na rasmi katika siku itakayopangwa na kuamuliwa”
“Tunaweza mtafutia Land Cruiser 200 Series na some other stuff kuonesha commitment yetu katika kujali na kuheshimu wajibu wake regarding tofauti zilizoonekana wakati wa kampeni, this is possible”
Baada ya kuulizwa kwanini alifuta post hiyo alisema anapaswa kuliweka jambo hilo katika vikao kwanza;