Lema tunahitaji maandamano,Watoto waliofeli kwenda sekondari ni kuibia fedha wazazi.

DT125

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
437
Reaction score
637
Hebu jiulize mwanafunzi akipata alama zote mtihani wa darasa la saba kwa masomo matano anapata 250, kwani kila somo linajumla ya alama 50. Miaka ya nyuma kwenda sekondari ilikuwa kufikisha jumla ya alama 100. Hii ilikuwa sawa na ufaulu wa alama 20 tu kwa kila somo, ufaulu ambao hauhitaji kupata nusu ya jumla ya alama. Kama ufaulu ungekuwa nusu ya alama mwanafunzi angelazimika kupata wastani wa alama 125. Kituko ni mwaka huu ambapo Dr. Shukuru Kawabwa pamoja na kudanganya kwa kusema kiwango cha ufaulu kimepanda wamelazimika kuchukua wanafunzi ambao wamepata alama chini ya 100 na kushuka hadi alama 70 hii ni sawa na kupata wastani wa alama 14 kati ya 50 kwa kila somo. Taarifa zisizo na shaka zinaeleza kuwa kwa alama za ufaulu za awali tayari kuna baadhi ya sekondari za kata zilikwisha kosa wanafunzi au kupata wanafunzi chini ya kumi huku sekondari nyingi zikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 120. Ni lazima utakubaliana na mimi kuwa kumlazimisha mzazi kulipa ada na michango mingine ya shule kwa kijana aliyepelekwa sekondari akiwa na alama chini ya 100 ni kumwibia pesa tu kwani kijana huyu hawezi kuvuka mtihani wa kidato cha pili. Kuna tetesi pia kuwa matokeo ya mtihani wa kidato cha pili ni mabaya sana. Ni wanafunzi wachache sana waliofikisha alama ya kufaulu ya 30. Kama serikali isipochukua uamuzi wa kushusha alama hizi walau kufikia 15 zipo shule za kata zitakosa wanafunzi wa kidato cha tatu mwakani. Tujiulize tunaelekea wapi?.
 
Mkuu halii hii kweli inahitaji nguvu ya mwanasiasa? kupambana na mambo kama haya, wizi ufisadi it begin with you no Lema or any body else. Kila kitu tukipeleka kwa wanasiasa ipo siku tutaomba maandamano pia ya kwenda kutongozewa na wanasiasa . Hatua za kuchukua unazo anza wewe ndipo mwanasiasa afuate
 
tuna andaliwa mambulula! kwa dunia ya ushidani hv cjui tz ya kesho itakuwaje
 
Wazo zuri lakini ww ni mwoga sana,kama ww hauna chembe ya woga basi ungeamasisha watu tukuunge mkono wakati utakapo anzisha maandamano ya kupinga wizara ya elimu na mapungufu yake. KATIBA yetu ya 1977 inakupa uhuru wa kudai haki kwa njia ya maandamano so yanini kuwa na kamanda Lema wakati nawe ni mtanzania huru na mwenye akili timamu? Kama unataka mabadiliko ya kweli hayatakuja kwa kuanzisha hoja na kutaka iongozwe na mtu mwingine. Kama umeanzisha movement lzm utake responsibility na wadau tutakuunga mkono.
 
Kama ni maandamano yaandaliwe Tz nzima bila kujali itikadi zetu ,kwa sababu kila mtanzania wa kipato cha chini ni Muathilika wa janga hili.
 
Back
Top Bottom