Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akiongea na wanahabaru hivi karibuni amezungumzia namna ambavyo kumekuwa na hujuma kwenye zoezi la uandikishwaji wa wananchi kwenye Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa.
Lema amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa serikali wanafanya mbinu ikiwemo kutengeneza semina maalum za kutoa maelekezo jinsi ya kuiba uchaguzi
"Wananchi wakishakata tamaa wakaona democracy is not an alternative, kuna siku watalipuka. Yaani system nzima ya serikali inakaa kupanga kuiba uchaguzi. Wanafanya semina za kuiba uchaguzi. Wanalipana posho za kuiba uchaguzi. Wanatoa maelekezo ya kuiba uchaguzi"
Soma pia: Freeman Mbowe ajiandikisha Uchaguzi Serikali za Mitaa
Lema aliongeza kwa kusema:
"Kuna baadhi ya vituo wameweka makada wao wa Chama Cha Mapinduzi hao wanafanya swapping. Unaenda kwenye kituo kutembea unakutana na msimamizi wa Uchaguzi ana hasira, akimuona kada wa Chadema ana hasira"
Mbona kama CCM wamepania sana. Kuna nini?