William Malecela (Le Mutuz au Baharia) ni mwanachama mwanzilishi na mmoja wa wadhamini wa kwanza kwanza kabisa wa jukwaa hili kuanzia 2005. Aliwahi kuwa na ID za Mzee ES na Field Marshal ES wakati bado anaishi New York City. Muda mfupi kabla hajaamua kurudi nyumbani alimua kubadilisha ID na kuweka jina lake halisi la William Malecela ingawa sasa hivi sijui anayumia ipi. Katika kipindi hiki chote hapa JF ametoa michango mingi sana ya maana, tumelumbana naye kwenye mada nyingine nyingi sana na kufikia kukubaliana kutokukubaliana, na vile vile amewahi kutoa michango ambayo ilionekana haifai kujadiliwa kabisa. Hayo yote ndio msingi wa majadiliano na ni kati ya chachu zilizosababisha JF ikubalike kwa watu wa mbalimbali katika jamii.
Wiki hii nimesoma kwenye mtandao mwingine kuwa amelazwa Muhumbili kwenye taasisi ya moyo; sijaona thread yoyote JF inayohabarisha jambo hilo, na kama ipo basi huenda ni obscure sana kiasi kuwa haionekani mara moja. Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba wana JF wote tumtumie salamu za pole mwanachama huyu mwandamizi wa jukwaa hili. Atakayeweza kumtembelea afanaye hivyo, atakaye mtumia SMS afanye hivyo na yule atakeyesaini kwenye thread hii kumpa pole asisiste afanye hivyo. Le Mutuz na mojawapo ya nguzo kubwa sana zilizojenga JF.
View attachment 1092909
Ugua pole mwenzetu Le Mutuz. Binafsi ninakuombea mwenyezi Mungu akurudishie afya yako yenye nguvu urudie kwenye majukumu yako bila kusita kutoa "Tamkoz"