Lengai ole Sabaya akutwa na ukwasi wa Tsh. Bilioni 3 baada ya kupekuliwa

Kwann takukuru hawakuenda kumhoji sabaya cuthbert alipolalamika? Au takukuru nao ni chimbo la ulaji?
 
Wateuliwa wa mwendazake wote ni mabilionea waliyoyapata baada ya kuimba mapambio huku wanyonge wakinyongwa wakishangilia propaganda feki
 
Nitafarijika sana kama mama ataamua kubadilisha fedha zetu tena haraka, ili katika historia ya fedha ya Tanzania kuwe na sura ya Mwanamke. tena awahi haraka!
 
Bashite alipiga pesa ndefu Sana kwenye vita feki vya unga huku Hakuna hata mtu mmoja kwenye list yake yupo ndani kwa unga.
 
Huo ni utopolo tupu hakuna cha habari hapo!!
 
Bashite alipiga pesa ndefu Sana kwenye vita feki vya unga huku Hakuna hata mtu mmoja kwenye list yake yupo ndani kwa unga.
Mmmh yaani huwajui walioko ndani na wengine wameshafugwa? Pia madawa hapa Dar yamepungua mno. Kinondoni watu wamepumua sana tu na madhara ya dawa mkuu au haupo Dar?
 
umeandika uzi mrefu sana ila kumbuka tunafanya makosa sana kukimbilia kuhukumu watu, tusubiri uchunguzi upite ahukumiwe kwa haki.
 
Huo ni utopolo tupu hakuna cha habari hapo!!
Hii habari kwa sehemu kubwa hasa hiyo ya billion 3 itakuwa ni uzushi wa kitoto sana. Na uzushi kama huu utamsafisha sabaya na kumfanya afanikiwe kukwepa mkono wa dola. Haya magazeti yakifungiwa yanalia lia ...
 
Vijana huwa wanajisahau sana wakipata madaraka!!
 
Ni kama vile walikuwa wanawakilisha gawio kwa mungu wa Burigi. Ndio maana walilindwa kwa nguvu kubwa, nao wakawa miungu midogo.
 
Ingawa ni kweli Sabaya alikuwa ni mporaji na jambazi lililojificha kwenye uvungu wa kitanda kinachoitwa ccm, ila hii taarifa siimani hata kidogo.

Bilioni 3 zote hizo amezipata wapi ndani ya muda mfupi wa U DC wake hapo Hai?
Na hana akili kiasi hicho aweke bilioni 3 kwenye droo ya kitatanda (nyumbani), hii taarifa si ya kuaminika sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…