Lengai Ole Sabaya alikuwa anatembea na dola za marekani tu, msaidizi wake ndiye alikuwa anapewa jukumu la kwenda kuzibadilisha mitaani, hizo fedha alizitoa wapi? ni dili la dhahabu alilowapiga wafanyabiashara fulani huko Hai ambao mapande ya dhahabu hayo walikuwa wameyaficha kwenye kiti na kuchomelea kisawasawa, kupitia vijana wake, sabaya alilikamata gari hilo na kumwamuru OCD gari hiyo ifanye doria kwa siku hiyo pasipo Sabaya kumweleza uwazi OCD wafanyabiashara hao walitaka kumuhonga milioni 50 hadi 100 OCD na kijana wa Sabaya ambaye aliwekwa kwenye doria katika gari hilo kimkakati kwa ajili ya kumpa sabaya taarifa zote zitakazojiri kutoka kwa wafanyabiashara hao, DSO alipopenyezewa taarifa hizo alianza kufuatilia taarifa hizo na dhahabu hiyo, lakini Ole Sabaya aliamuru DSO huyo ashughulikiwe na vijana wake, na DSO alipigwa sana hadi akapelekwa kulazwa hospitali, Sabaya aliichukua ile dhahabu yote ikawa mali yake binafsi, DSO alipotoka hospitali aliandaa report yake akaituma hadi kumfikia Rais, Magufuli alimuita Sabaya ikulu akamhoji kuhusu tuhuma hizo, lakini Sabaya ili kumfurahisha Magufuli akamweleza kwamba ni fedha siyo dhahabu zilizokuwa zimepelekwa Hai na Mbowe ili achukue jimbo yeye akawa amezikamata.....mambo ni mengi sana....lakini naona faili lake lilisahulika mezani kwa Rais hadi Samia kulikuta.
Vile vile, jiulize ni kwa nini wilaya ya HAI ilikuwa ni ya 5 -6 katika kukusanya mapato ya serikali, ukishajua ndo uelewe umafia mwingine wa sabaya aliowafanyia wafanyabiashara ili kumfurahisha Magu