Lengai ole Sabaya akutwa na ukwasi wa Tsh. Bilioni 3 baada ya kupekuliwa

Lengai ole Sabaya akutwa na ukwasi wa Tsh. Bilioni 3 baada ya kupekuliwa

Gazeti la Raia Mwema la Jumamosi, 15 May 2021 limeripoti kuwa DC aliyefurushwa huko Hai, Lengai Ole Sabaya (34) amepekuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama na kukutwa na ukwasi wa zaidi ya TZS 3 Bilioni.

Kwa mujibu wa gazeti hilo baadhi ya fedha zimekutwa nyumbani kwake na nyingine kwenye taasisi mbalimbali za fedha.
Dah..mzalendo mchapakazi aliyefananishwa na hayati Sokoine!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu DC apelekwe mahabusu Kwanza ili uchunguzi upitie na kupata taarifa rasmi,anapokuwa huru ataharibu Kila kitu kwa wtz hawakubali kushindwa.
 
Kuna kitu kinashangaza, baada ya JK kutoka madarakani watu walizungumza mazuri yake na mabaya kwa kheri kabisa.
Lakini Magufuli mazuri yana zungumzwa kwa kulazimisha na mabaya yakitajwa yanabishiwa kwa matusi na ghadhabu kuu mno kwa nini?
Nafikiri kwa Magufuli kuna kasoro kubwa ndio maana inatumika nguvu kubwa kuficha mambo
Udini umetabaruki kila kona nchi hii,Maroli yote Ni waislamu,tumechoka tunataka equality.
 
Si Alikuwa na mshahara?
Mshahara wa milioni 5 kwa mwezi ndiyo ukufanye umiliki bilions!! Hata ujitetee kufanya biashara, bado siyo kazi nyepesi kuzikamata hizo bilions ndani ya muda mfupi.

Only through fraud, embezzlement, corruption, piracy, plundering, looting, robbery, etc can be possible!
 
Hizo taarifa za gazeti sio rasimi,mpaka polisi waseme kuwa wamepekua ndani na wamekutana na vitu furani,kumbukeni ni juzi tu taarifa za kigogo mmoja zilisambaa kuwa amekutwa na fedha nyingi na fedha za nje Dola 150.lakini polisi ilikanusha na wanasema tuzipuuze hizo taarifa.
 
Kayafa alikuwa ni fisadi wa kiwango cha bulldozer aliejificha kwenye propaganda za kuchapa kazi!
1621258979442.jpg
 
Gazeti la Raia Mwema la Jumamosi, 15 May 2021 limeripoti kuwa DC aliyefurushwa huko Hai, Lengai Ole Sabaya (34) amepekuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama na kukutwa na ukwasi wa zaidi ya TZS 3 Bilioni.

Kwa mujibu wa gazeti hilo baadhi ya fedha zimekutwa nyumbani kwake na nyingine kwenye taasisi mbalimbali za fedha.
Raia mwema limekuja ki propanga Zaidi.
 
Back
Top Bottom